Sunday, July 15, 2012

TUNAPANDA ...


Asanteni kwa vile ilisemeka kama musiki safari,na mengineyo mengi..lakini kumbe kwenye safari kuna njia maana unaweza kuulizwa unaelekea wapi?hapo kuna njia..kama ni msanii basi unaelekea kuwa msanii bora kitaifa ama kidunia kabisa,sijawahi ona msanii anaulizwa anamatarajio gani katika fani yake na y eye akasema anataka awe anajaza bia na vilevi vingine kwenye friji,kwa maana mengine si ya kuuliza,
hapo huyo akiwa amekosea njia,na kama anakuwa amepatia basi mmoja anaweza fanya ili baadaye aje asome tena,maana hayo ndiyo mabonde,pengine baadaye ibadilike na kuwa milima,maana kuruka sio kama kupanda,inakuwa taabu sana kutafuta kitu ulichokuwa nacho bila kujua,labda ujue kinachokuja..

Maisha ni yamejawa na yote yaliyomo humu,pengine duniani ya  kuwa siyo yote nitakayo yasema,ama pengine wewe kunielewa,maana mengine nitayapandikiza,leo hii watoto yatima wamejaa sana mitaani,hii ikiwa sio kazi yako ni ya serikali,hata kama na wewe pia ni serikali basi jaribu kulea mmoja,maana wenzetu wanawanunua hao,hii nadhani ndiyo maana ya mlima kilimanjaro kuwepo Tanzania,maisha yamekuwa magumu sana mpaka hata watu hawajielewi wenyewe,maana kama hutaki kuzaa kataa elewa pale unapoambiwa..

Katika kuyafahamu maisha ni kujifahamu wewe mwenyewe,maana jikataze pengine ukiwa hupendi kupanda panda milima,unapoelewa kama mlima upi ni mzuri na wa faida elewa pia na mwengine ulio mbaya,maana pengine ndiyo maana tunabadilika..wacha na mengine yabadilike.nakaa nikiamini kesho tutakutana kileleni,nakaa  nikiamini milima mingi maishani
Bado tunapanda,bado tunapanda milima..

MSEMEA MWENZA..!


Uwezo unatofatofautishwa zidi na yule  atendaye hivyo,sema wewe mwenzako bado hajaweza,eleza wewe ya mwenzako siyo ya kuyatenda,maana hapa tunataka kuona wewe,yaani uwezo..ndiyo ikiwa inahitajika namna ya kuonyesha kwamba ile ilikuwaje,katika mwanzo kuna mwisho,na isingekuwepo hata tusingetamani,maana si ingekuwa tofauti na sasa?pengine tutamani wenzetu wanavyosema,ikiwa ni kutaka kukuza uwezo wako,lakini tukisema yao tutaonekana wambeya,pengine wengine wanafanya yao tuseme,ama tunajisemea tuu,na endapo ikifika wakati itaonekana   tumeshindwa ni kwa sababu hatukusema yetu.

Hapa anatafutwa Yule ambaye amemsemea mwenzake,maana katika kipindi cha kuonekana kusema hakuonekana msemaji na baadaye ikaja bila ya kuelewa,pengine ni nafasi yetu,mwengine ni nafasi yake,haina maana ya kuomba ruhusa wakati hatuna hitaji nalo,tena isiwe tunatega,isieleke namna ya ilivyo mtego ikawa ni kama ombi,hapa na pengine yatupasa kuelewa.

Sema mwenyewe maana hakuna wa kukufanyia,fanya kwa nguvu kwani ni nguvu zako zitakazo sema ,hapo kukiwa hakuna woga maana yamesikika mengi na hakuna kilichofanyika,hakuna yaliyotendeka kwani  wengine walidanganya,unaweza kufanya kwa nguvu lile lililo na uwongo hapo kushindwa kueleweka,maana hata wanaomsemea mwenzake wanasubiri neno ili  mradi limesemeka ili kuonekana wao wanaweza,tutajua linalofuata kwa matokeo yanayokuja,maana si tumechagua kusema wenyewe?
hapo labda tuseme ya kwetu maana kama yakiwa ya watu tutakuwa wa kwanza kwa kutokuya weza,fanya yako..


MBISHI.

Mbishi ndiyo huyu huyu unayempa heshima kila siku,tena wapo wengi,kwa maana ukaamke asubuhi na kuandaa heshima zao,hapo katika heshima wale wanaobisha huwa ni wakubwa,hata katika kubisha ikiwa katika hali ya kawaida kwani ukifiri haina maana ya kuwepo mkubwa na mtoto,haina maana ya kuwepo heshima,maana kama ulijitolea nguvu zako kuwalisha watoto wako na sasa ukabisha kwa kuwa na matendo yasiyoendana na ulimwengu  basi utakuwa umebisha mwenyewe,na hivyo ni lazima upokee lawama kwa hao uliowazidi,maana wao hawajui kitu,labda vile watoto wanaelewa kwa namna ya vile ilivyo,mkubwa akabisha kwa namna ya kujua kile cha utoto.huku akijua chake.

Mara nyingine watu wengi hufikiri nafsi za watu kama za kwao,hawaelewi kama kubisha kwao ndiyo nafsi za watu wengine,wabishi wanaweza kukufanya hata kufa,kwani ukifikiri kwa uwepo labda utakuwa unafahamu lakini kwa yaliyopo imeonekana ukibahatisha kwa kutokujua lile wanalobishia wabishi.maana mbishi akibisha amemaanisha kujua zaidi,kuwa mbishi ni vyema hasa katika maisha haya ya kisasa,lakini ni lazima ieleweke kama unayabishia nini,tena ikiwa kwa kuyaelewa.

Ubishi raha sana,ukiwa mbishi ni lazima uwe na kumbu kumbu ya kutosha,maana kesho itafika utaambiwa neno lile lile,ili kutaka kukutega,kuzunguka hakuna mwelekeo zaidi ya mzunguko,maana hata hiyo kulia na kushoto ndiyo inayoleta ubishi zaidi,dunia inazunguka na sio vile inaelekea kushoto ama kulia ama hapo utabishana ukiwa haujui kweli.

KIZUNGUZUNGU...


Kizungu zungu kinachanganya sana,maana kwa mtu kuwa mkubwa naye anatakiwa aongee kizungu,ndiyo hapo watu wengi hupata kizunguzungu,kizunguzungu sio ya maana ya kuchanganyikiwa,heli ingekuwa kukuchanganya kuliko kizunguzungu,maana itafika mwisho uelewe kwamba kinachoitajika ni kizungu,sio kuzunguka zunguka.maisha yanaweza kukuweka ukawa katika namna ya kizungu zungu maana yenyewe hupenda kwenda na kurudi na Yule anayeyazungusha ni wewe,sasa ikawe umependa kuzunguka sana lazima ujue kizungu,hapo usije kuchanganyikiwa kwa mizunguko ya maisha iliyopo..

Hakuna kile kilicho cha zaidi,zaidi ya mtu mwenyewe,unapoamua kuanza ndiyo pale mwisho wako unaweza kujulikana,maana mwishoni tunataka kuulizana..wewe umefanya nini,pengine hapo ndiyo tukajua kama kizungu kinafahamika,maana zile YES au NO utaona zikitamkwa kwa namna tofauti,bado hapo tuleteane kizunguzungu maana sio wote watatuelewa,na hata kwa mmoja usitegemee kueleweka  mwanzoni,maana katikati kuna miiba,na safari bado haijaisha hii.

Leo tumetawaliwa na lugha tofauti sana,wale wa kizungu tumejitawala kwa lugha tofauti sana,haki ya mtu kujitawala.jitawanye mwana dunia ni yako..hizi ni kauli chache kwa baadhi wanapoweza,maana unaweza kufanya jambo kwa kurudi nyuma,hapo ukiwa hautembei,hata kama kutembea ni kwenda mbele na nyuma,basi chagua kutembea nyuma,hapo utaona namna ya kizunguzungu,ikiwa ni kurudi nyuma..kwa kushindwa kuelewa  maana tu.maana unaenda enda tu,kama unakizunguzungu vile.tunagalie haya ya leo kwa maana ya kesho,isije kuwa ya leo ya leo tu..

HUKUMU...


Naizungumzia nafsi nikihusisha hukumu,naizungungumzia haki inapotoka hukumu,hukumu inapotoka hakuna namna ya kuweza kutoroka,kwani matendo yako ndiyo uwanja ambao umesimama,hatuwezi kukimbia yale na vile tulivyovifanya,mara nyingine tunaulizwa kwanini umefanya vile kwa maana wakiwa hawaelewi au wanaelewa tofauti,maana vile mtu wakasema Yule anakejeli lakini uwazi ni kaelewa tofauti.

Maisha yanatakiwa kuishi na kuwa,unaweza wakati mwingine ukachoka kuona watu,na hiyo ni kwa sababu ya nafsi yako inavyosema,kama vile usemavyo habari ya maana ya kumsalimia mtu pumzi yako ndiyo inaweza kusema,tukatambua umesema nini,utakapo gundua mahala ulipo,kuna muda mwingine hatuelewi kama tunafanya mazoezi ya maisha yetu,tunaishi ni kwa sababu hatujui tunaishi vipi ila tukiwa tunataka nini,pengine tubadili lugha za kuomba na kusema nataka,ikiwa hatujajua ya huko nyuma basi haina haja ya kufikiri uko huru,maana yahitaji kutoroka mahala tulipo sasa.

Ni wazi kujitambua,ikiwa haina njia mbadala wa kutoroka afya yako,maana utakuwa umekimbilia kifo,ni namna gani ambavyo tutaweza kutokukimbilia kifo hapo nikuviweka tofauti,kati na kukimbia na kutembea,maana tumeambiwa tutembee ili tuwe na uangalifu mzuri,pengine wenzetu wanafundishwa vizuri sana,ama ni kuimba ama kucheza mpira,lakini ingali hapo na wengine hawajui,sidhani kama linaweza kuwa darasa zuri,maana watakuwa wachache wameamua kutuchagulia maisha yetu,tukijiangalia katika matokeo ya hukumu zetu ni namna yetu vile tunavyokuwa,hapo tutaijua hasira na asili ya maana tulipo,nikikumbuka muda watu tunasema tunahasira na maisha.pengine tuangalie maana hukumu kila mtu na yake.






ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...