Kizungu zungu kinachanganya sana,maana kwa mtu kuwa mkubwa
naye anatakiwa aongee kizungu,ndiyo hapo watu wengi hupata
kizunguzungu,kizunguzungu sio ya maana ya kuchanganyikiwa,heli ingekuwa
kukuchanganya kuliko kizunguzungu,maana itafika mwisho uelewe kwamba
kinachoitajika ni kizungu,sio kuzunguka zunguka.maisha yanaweza kukuweka ukawa
katika namna ya kizungu zungu maana yenyewe hupenda kwenda na kurudi na Yule
anayeyazungusha ni wewe,sasa ikawe umependa kuzunguka sana lazima ujue kizungu,hapo
usije kuchanganyikiwa kwa mizunguko ya maisha iliyopo..
Hakuna kile kilicho cha zaidi,zaidi ya mtu
mwenyewe,unapoamua kuanza ndiyo pale mwisho wako unaweza kujulikana,maana
mwishoni tunataka kuulizana..wewe umefanya nini,pengine hapo ndiyo tukajua kama
kizungu kinafahamika,maana zile YES au NO utaona zikitamkwa kwa namna
tofauti,bado hapo tuleteane kizunguzungu maana sio wote watatuelewa,na hata kwa
mmoja usitegemee kueleweka
mwanzoni,maana katikati kuna miiba,na safari bado haijaisha hii.
Leo tumetawaliwa na lugha tofauti sana,wale wa kizungu
tumejitawala kwa lugha tofauti sana,haki ya mtu kujitawala.jitawanye mwana
dunia ni yako..hizi ni kauli chache kwa baadhi wanapoweza,maana unaweza kufanya
jambo kwa kurudi nyuma,hapo ukiwa hautembei,hata kama kutembea ni kwenda mbele
na nyuma,basi chagua kutembea nyuma,hapo utaona namna ya kizunguzungu,ikiwa ni
kurudi nyuma..kwa kushindwa kuelewa
maana tu.maana unaenda enda tu,kama unakizunguzungu vile.tunagalie haya
ya leo kwa maana ya kesho,isije kuwa ya leo ya leo tu..
No comments:
Post a Comment