Sunday, July 15, 2012

TUNAPANDA ...


Asanteni kwa vile ilisemeka kama musiki safari,na mengineyo mengi..lakini kumbe kwenye safari kuna njia maana unaweza kuulizwa unaelekea wapi?hapo kuna njia..kama ni msanii basi unaelekea kuwa msanii bora kitaifa ama kidunia kabisa,sijawahi ona msanii anaulizwa anamatarajio gani katika fani yake na y eye akasema anataka awe anajaza bia na vilevi vingine kwenye friji,kwa maana mengine si ya kuuliza,
hapo huyo akiwa amekosea njia,na kama anakuwa amepatia basi mmoja anaweza fanya ili baadaye aje asome tena,maana hayo ndiyo mabonde,pengine baadaye ibadilike na kuwa milima,maana kuruka sio kama kupanda,inakuwa taabu sana kutafuta kitu ulichokuwa nacho bila kujua,labda ujue kinachokuja..

Maisha ni yamejawa na yote yaliyomo humu,pengine duniani ya  kuwa siyo yote nitakayo yasema,ama pengine wewe kunielewa,maana mengine nitayapandikiza,leo hii watoto yatima wamejaa sana mitaani,hii ikiwa sio kazi yako ni ya serikali,hata kama na wewe pia ni serikali basi jaribu kulea mmoja,maana wenzetu wanawanunua hao,hii nadhani ndiyo maana ya mlima kilimanjaro kuwepo Tanzania,maisha yamekuwa magumu sana mpaka hata watu hawajielewi wenyewe,maana kama hutaki kuzaa kataa elewa pale unapoambiwa..

Katika kuyafahamu maisha ni kujifahamu wewe mwenyewe,maana jikataze pengine ukiwa hupendi kupanda panda milima,unapoelewa kama mlima upi ni mzuri na wa faida elewa pia na mwengine ulio mbaya,maana pengine ndiyo maana tunabadilika..wacha na mengine yabadilike.nakaa nikiamini kesho tutakutana kileleni,nakaa  nikiamini milima mingi maishani
Bado tunapanda,bado tunapanda milima..

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...