Sunday, July 15, 2012

HUKUMU...


Naizungumzia nafsi nikihusisha hukumu,naizungungumzia haki inapotoka hukumu,hukumu inapotoka hakuna namna ya kuweza kutoroka,kwani matendo yako ndiyo uwanja ambao umesimama,hatuwezi kukimbia yale na vile tulivyovifanya,mara nyingine tunaulizwa kwanini umefanya vile kwa maana wakiwa hawaelewi au wanaelewa tofauti,maana vile mtu wakasema Yule anakejeli lakini uwazi ni kaelewa tofauti.

Maisha yanatakiwa kuishi na kuwa,unaweza wakati mwingine ukachoka kuona watu,na hiyo ni kwa sababu ya nafsi yako inavyosema,kama vile usemavyo habari ya maana ya kumsalimia mtu pumzi yako ndiyo inaweza kusema,tukatambua umesema nini,utakapo gundua mahala ulipo,kuna muda mwingine hatuelewi kama tunafanya mazoezi ya maisha yetu,tunaishi ni kwa sababu hatujui tunaishi vipi ila tukiwa tunataka nini,pengine tubadili lugha za kuomba na kusema nataka,ikiwa hatujajua ya huko nyuma basi haina haja ya kufikiri uko huru,maana yahitaji kutoroka mahala tulipo sasa.

Ni wazi kujitambua,ikiwa haina njia mbadala wa kutoroka afya yako,maana utakuwa umekimbilia kifo,ni namna gani ambavyo tutaweza kutokukimbilia kifo hapo nikuviweka tofauti,kati na kukimbia na kutembea,maana tumeambiwa tutembee ili tuwe na uangalifu mzuri,pengine wenzetu wanafundishwa vizuri sana,ama ni kuimba ama kucheza mpira,lakini ingali hapo na wengine hawajui,sidhani kama linaweza kuwa darasa zuri,maana watakuwa wachache wameamua kutuchagulia maisha yetu,tukijiangalia katika matokeo ya hukumu zetu ni namna yetu vile tunavyokuwa,hapo tutaijua hasira na asili ya maana tulipo,nikikumbuka muda watu tunasema tunahasira na maisha.pengine tuangalie maana hukumu kila mtu na yake.






No comments:

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...