Sunday, March 18, 2012

Tutafurahia ushindi kwa kusherehekea tuliyoyafanya...


Panapokuwa na sherehe sio lazima kuwe na ushindi,pengine unaenda katika sherehe kwa vile furaha uliyonayo,pengine ukafanya kusherehekea mabaya na bila kujiuliza mazuri ni yapi
unapoenda sio kule ulipokuwa,ikafika kipindi ukaelewa maneno ikiwa maana yenyewe imekuwa ni ile ile inayojirudia,kipindi kitafika atapewa mshindwa ushindi,
na
hii ikiwa sio kwamba umefanya tofauti bali ni namna ya vile mshindwa alivyoshindwa kashinda,maneno yalipangika tokea muda ikiwa na lile analoliweza mwingine mwache,na ijulikane ushindi huleta furaha iwe ni kwa mshindwa ama aliye shinda kwani wote ni washindi katika namna moja mama ingine.

namna ya kuweza kushinda ni ile ya kuweza kufanya yaani ikiwa alifanya Fulani akaanza moja kwa kushika namba na mwingine akaja akiifuata na mpaka mwishowe ikaonekana nafasi ile ameishika mtu wa mwisho basi naye ameshinda,tatizo litakuja ikiwa itafanyika sherehe isiyotambulika kwani sherehe na zenyewe hulenga ikiwa ni sherehe ya ushindi wa ngapi au  wa ngapi

Chuki haina haja ya kuidhania,na ikiwa imesekana sio kwamba ipo bali ilifikirika,kwani na yenyewe chuki hutambulishwa kwa maneno na hata sura ikaonekana hivyo yaani kichukichuki,sura ya chuki haifichiki ziadi ya ile inayopendwa,

yale yanayoonekana ndiyo yanaumba sura yako kwa majibu yanayotoka moyoni na katika fikra zako,maana inaweza kutokea kipindi ukaambiwa mbona hufanyi kitu wakati unafanya,hapo watu wakitaka kushinda kwa namna yao,na ikiwa utaendelea kufanya hapo utakuwa mshindi na hayo kujulikana kama ni matokeo tu,kwani matokeo hubadilishwa kulingana na namna ya vile wachezaji wanacheza,ikiwa ni tofauti na ilivyo na kwa wachezaji basi hapo matokeo yanakua hayajabadilika,ndiyo vile kufurahia ushindi usio kuwa na furaha,tena na ikaitwa ni sherehe.

Jukwaa ni kwa ajili ya kuelezea ikiwa ni wengi wasikie,sio lazima ukawa ushindi yaweza kuwa burudani,ningalisema ni ushindi lakini ulishauzungumzia zamani sana mpaka ikafika kila mtu akawa na wake,la zaidi ni usijione kushinda kwani yule anayeshinda akitaka kuonyesha akiwa jukwaani hufika mahala na kupayuka,ushindi wako ukafuatana na uelekezi wa sauti,

wengine walioandaa sherehe wakataka watu wao ndiyo waelekeze sauti wakiamini ni sherehe baaadae bila kujua ile iliyopo ndiyo sherehe tosha nyingine inayokuja bado haijaja labda uitegemee tu kwani ikitegemewa sana hapo watu wanaweza kutaka kushinda bure,kushinda bure kuna kwingi hapa kuna kushinda bila kula,bila kufanya kazi au hata kwenda kazini na usifanye kazi yoyote si mshahara unaingia,na ubaya wa makaratasi huwa yanachanika,hapo ndiyo jukwaa litakapotanuka,utasikia maana wale wasafishaji wa vyakula vilivyotumika katika sherehe ya muda uliyopita hawakulipwa nao

Sherehe zimezidi kuwa nyingi na hapa imekuwa na maana ya kuwa mambo ya kufanya yameongezeka,tena ingali watu ni wale wale itakuwa wamekuja na namna tofauti,hili si la kuambiwa zaidi ni kulitambua,ushindi mgumu ndiyo ushindi maaana ya yule anayebisha autafute,kama iwapo mbaya vibaya,ikiwa ni mbaya nzuri.Muda unakwenda sasa na utambue utapamba nini katika sherehe ikiwa umepanga kusherehekea.

By:benson G.Makaya
Tel;+255714 3366 57
Email:bensonsmakaya@gmail.com

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...