Wednesday, June 27, 2012

HAKI YANGU..

Haya  yangu
Tanzania isiwe ni nchi ya kulalama,eti tukataka kufanya kwa kusema ni haki,pengine kila mtu yapasa kufahamu haki yake,haina maana ya kuumia na kulalama kwa nini umeumia,hapo hatutatumia udikteta,hapo hatutafanya maonevu,pengine kwa yaliyo machache tusifanye roho zetu zikawa siasa,hapa lazima tuelewe siasa ni nini,maana kwa pengine jana ikatokea mtoto wa jirani amejikwaa basi utasikia chama chao  hao,kesho ikija tunasema aaah hawa watakuwa wamelipizia,tukiwa tunaenda na kusema tunajengea watoto wetu maisha,hapa tutakuwa tunajijengea makaburi kwa bila ya taarifa,maana wengine wataona haina haja hata ya kukuzika,watachoma moto tu.

Kesho jamani ije bila ya kutokusahau,maana mengine wamekuja leo wakiwa wameumia sana.tufikiri hapo mwanzo kama tulikuwa hatulimi,leo hii tunaambiwa ni kilimo kwanza,ni kweli hata iliposikika,inaleta maana ya kuwa imemlenga Yule anayeambiwa,maana hata mtu ukakubari ndiyo lazima tufahamu kwamba kesho itatokea lake,wengine hawana hata kazi,eti tunasema hawaja soma,hawa wengine waliosoma ndio wanapigwa ili kuonyesha haki,nani apigane?maana mwenye haki asiyesoma,mimi yangu haya mwenzangu na mimi sijui haki yako iko wapi,tena angalia usije zikwa mzima.

Pengine nchi yetu imekuwa tambala bovu linalongoja matope yaje ilki kuyazoa,yakija masafi si wanasafisha wenyewe,tena huwa si vurugu kwani huitwa ruzuku,wanagawana wachache tu,wasichoke wengine kutupa msaada,wachoke wengine wenye kumaliza misaada,maana imetokea mkubwa kajua kama mkubwa kajua unadhani patakalika?

Haki yangu nitaifurahia mwenyewe,haki yangu haipaswi kwenda kama kifaranga na mwewe,leo isiwe lakini kesho itakuwa,haya ni yangu yamependezwa ingawa tunaangamizwa,kubali mdogo ndiyo wakubwa walivyotufundisha,kubali mkubwa ndiyo wadogo wanachostahiri,chukua chako ondoka,maana vengine vya wengine,
Haya zenu jamani...!!

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...