Friday, June 1, 2012

LULU-(Toleo maalum)

Zaidi ya vile upendo wangu kwako,umezidisha nafasi na namna ya kuweza,
umeniwezesha pale palipokuwa pagumu umenipa ujasiri hata wa kutokukwambia,
maua mazuri yanamwagiliwa japo ulifanya kujimwagilia,
umekuwa kiongozi wa wale wengine na kwangu pia,
hakika ntakupenda daima,kuwa na mimi karibu zaidi nizidi kuelewa,
ni mwanadamu gani asiye na hasira au za kwako usifanye mbele yangu,
ni heshima tosha,ni ujumbe tosha,umefanya yaliyokutosha 

haki akienda mtu tumwalakishe awahi maana nafasi zinajaa,
watu wanataka kumiliki vyao ikiwa baadaye isiwe taabu,
usinifanye nilie zaidi kwani yanatosha nasema tena,
nimekupenda kukupenda,nimefurahi kukupenda,maana pengine hata kwa mwingine isieleweke,
tujaribu kuinuka pamoja,tujaribu kuwa pamoja si kwa mda huo tu uliopangwa basi tuendelee,tukue,tuzidi mapana yaliyokuwa na ncha,
yasiyokuwa hata isiwe kwetu wakali,

maisha kuyatoa kwa mwana ni vyema kuliko kwa mwana,maana zikazalika ili jambo lile lije,ama kweli wewe ni mama yangu,ama kweli wewe ndiye unanifaa kukupenda,
pengine ni muda wako,pengine ilistahili kutokea kwa mara ya kwanza,
maumivu unayonipa si haba pale napojaribu hata kushika simu na kukupigia,hapo ninakuwa nimekumiss yaani kukumbuka,nakukumbuka sana mpenzi wangu,huwa nakukumbuka sana uwepo wetu wa pembeni,maana huwa tunazungumza sisi tu,
sisi ndiyo kumetufanya tuwe hapa,tumefika bila kujali vitu,ingawaje umekuwa kama ngao lakini ujasiri wa kuyachukua maisha yangu pia umekuwa nao,maana asidanganye mtu kwa kusemea mwingine,
fikiri hayo haraka kwa kuchagua wengine,
maana wa leo ndiyo asili,wa leo ni wa leo tu,wa leo ndiyo ametimilisha haya,mama yangu mpenzi umenikuza,baba yangu mpenzi umenilea,ndugu zangu wapendwa tumekuwa pamoja,
maana kuna kukosea na tukasema pale ilikuwa vile na sio ulifanyaje kwa kutaka kujua,umebaki lulu kwa yote,umekuwa dada yangu mpenzi,
sasa na milele ntazidisha mapenzi

KUNENEPA..


Pengine ukawe umemaliza mambo yako,au ukawe upo katika njia ya kuutaka ufalme,kipindi kile cha ngamia kupenya kwenye tundu la sindano si sawa na unene kwa maisha,kwani pengine umezaliwa mnene,au umekuwa hivi,pengine hupendi kuwa mnene,pengine ni hitaji la mwenyezi mungu kunenepa,hapa ukafikiri umeridhika huku ukiendelea kutafuta,unatafuta vingi labda isiwe kwa mtafutaji,anayetafuta sio mnene wala mwembamba,anayetafuta anataka hivyo,anayepata anaweza kuwa hakutaka kutafuta namna hiyo,pengine haikupendeza machoni pa moyo kwa wale wanaotenda mbele za watu,maana huwezi kuchuna watu ngozi na kuwakata viungo ukisema tunatafuta jera,wengi wetu huwa wamekosa amani ya moyo katika kuona maisha yao,wao wanakuwa ni kama ngamia wanene kwenye tundu la sindano,fikiri ngamia kunenepa,fikiri ngamia kunawili,fikiri ngamia mtaabikaji kutoka jangwani na kuishi nji kavu..

Pengine ni hizi hali za hewa zinazobadilika kwa mara inapobadilika,ikiwa ni hali  yenyewe au hewa ikaja bila ya kuwapo hali Fulani,hapo yakaja mafuriko,tena watu wasife ila waone,ili nao wao wakajiandaa na mafuriko,ukisema kesho upigane kuna wengine hatutajiandaa vizuri na ikija vita ndiyo tutakufa vizuri,lakini uijue maana ukapigane ya nini na kama hutaki hivyo basi unenepe ukiwa umeridhishwa na matakwa yako na asikuchagulie mtu unene,wako ndiyo mti mwema kwani ukiumwagilia vyema ndiyo uwingi wa matunda katika kuujaza mti.

Hakuna mtu anayekatazwa kuridhika,hakuna mtu anayekatazwa kunenepa hakuna mtu aliyesema kuwa mwembamba ni bora,kama na endapo lako limeonekana basi timizia haja,liweke likiwa limetendeka endapo kuna mapenzi nayo,hapo ikiwa chaguo limehusika,pengine ukataka sio chaguzi lako na usishangae ukikonda,usishangae kuona tofauti ya vile ndivyo,ndivyo ndiyo vile ya vile itakiwavyo yaani kwa mtu ikaleta kuridhika ikiwa imetarajiwa hivyo,furaha mtu hakupi bila yake,yako ni njema ya kuwa si ya mtu,hapa ukaridhika ya kuwa raha tunajipa wenyewe,raha ni lazima kuisubiri,raha zipo nyingi ni kusema ipi ni bora na mwingine akasikia ikiwa mwengine haijui shida,Yule wa mwisho atatenda tu tena ikiwa ni kwa kusubiria akitaka kunenepa.

Kumbe pengine hatutaki kunenepa zaidi ya  kubadilika,hapa unahitaji mabadiliko kama ulikuwa unapigana basi usipigane,kama ulikuwa hupigani basi usipigane,maana kwa mazuri huja baada ya mabadiliko,kubadilika ni kwenda na muda kama vile giza linavyokwenda na nyakati zake,likatoka na usiku kuwa mnene,usiku ni mwembamba yasemekana maana hilo nene lisingetokea,hapa tutabadilika hata kwa lazima,maana maisha ndiyo yanasema hivyo,kama kuna waliosikia basi na wengine watende ila uangalie usitake kunenepa kwa kutamani,maana matamanio nayo huja kimabadiliko,yenyewe huwa yanaenda na siku tunaita fashion,kumbe nyengine mbwembwe tu kiachohitajika ni kwenda na fashion.

SIJUI..

Kwa muda mwingine huwa nawaza niandike nini lakini kwa sababu zingine huwa nawaza kwa nini sababu za nini?maana mengi ya duniani ndiyo ya vinywani,mengi yakusemeka,mengi ya duniani ndiyo yale kawa maandishi,pengine tukajua huko.pengine tukaona ni nini kipo huko,tukisema sasa tumerudi hapo tutaulizwa tulikuwa wapi,hapa tuweke sababu,hapa tudanganye tena ikaaminike,isije aminika ya kuwa ndivyo ilivyo bali iaminike ya kuwa ndivyo ulivyo,sio kutafuta ni kufanya,sio kufanya ikaeleweka,sio kueleweka ikawa imetafutika,hapo sababu zitakuwa nyingi  sana,hapo tutashindwa kujiuliza na kujiuliza na kujipa majibu,tena ndiyo haswa tueleweke kama hatujaelewa kwa maaana ya kushindwa tena labda hatukusoma  vizuri ama yalikuwa tu hayaeleweki kwa kubisha,sisi wengine ni wabishi sana,sisi wengine ni watata sana,hata kama maneno yanafanana,kwa machache lazima kuelewana.

Muda  hauji ukaja ukasema,muda unasema wenyewe kwani ni lugha nyingine pengine wakaelewe wale waizungumzayo lugha hiyo,katika kujifunza kuna kujua endapo mtu amefahamu,akiwa amejua au hata amehitaji kutambua,najua tumechoka sana,pengine tukiwa tunahitaji lakulifahamu kulingana na huo muda,pengine ni sisi wenyewe wa kujifahamu maana hata huo muda ukawa hauna maana,kwa kuwa mdogo ama kupungua katika yale yanayotakikana

Hakuna mtu anayependa kuchelewa kama sio kuwahi sana.pengine watu wameshangaa kuona mwezi wakati wengine wakiwa na hitaji la jua,wakilitafuta kwanilinasikika tu,wengine wachache walilliona wale tunawaita wazee tena wazamani maana siku hizi kuna wazee wakisasa,hapa sijui tuliuchelewa  muda ama tuliona tofauti,au pengine ndiyo namna halisi ya ilivyo..ilivyo maana na namna ya mtu akatambue akaishi vipi,ilikupata moja lazima kufikiri na mwisho,kwani sio tatu pekee ni bora,hata kumi pale ikawa bahati nasibu.na hapa watu wanabahatisha sana na kusema wameweza,hiyo ikiwa ni imani ya kutaka kuweza na kushindwa.

Mwisho wa kumalizia ndiyo mwanzo wa jambo,ikiwa tu limeonekana,limesikika hapo kutakuwa na mwisho na mwanzo tusiufahamu,tena tukasema kwa yale tunayoyafahamu na kuyaweka kweli,hapa huwa tunaongea sana,huwa tunajiona tumeweza tusipojua hitaji ni tofauti maana tusingeweza kuwaza pamoja,hapa isinge kuja ile namba moja,ikiwa hivyo tunahitaji umoja,maana kwa umbali tusijifanye zaidi hata tukasikilizana,hapa lengo ni kuelewana,kwani hata ingekuwa namba zinajipanga zenyewe sidhani kama mbili ingependa kukaa nyuma ya moja na wakati yenyewe ni kubwa,fikiri kuwa na nyumba mbili na mija pale unapohitaji,pale unapokuwa na kitu chako kimoja fikiri mbili kuwapo kama si furaha ndani yake,labda isivyo amani kwa yale mabaya kwa mwengine.tumalize kwa kumaliza.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...