Friday, June 1, 2012

KUNENEPA..


Pengine ukawe umemaliza mambo yako,au ukawe upo katika njia ya kuutaka ufalme,kipindi kile cha ngamia kupenya kwenye tundu la sindano si sawa na unene kwa maisha,kwani pengine umezaliwa mnene,au umekuwa hivi,pengine hupendi kuwa mnene,pengine ni hitaji la mwenyezi mungu kunenepa,hapa ukafikiri umeridhika huku ukiendelea kutafuta,unatafuta vingi labda isiwe kwa mtafutaji,anayetafuta sio mnene wala mwembamba,anayetafuta anataka hivyo,anayepata anaweza kuwa hakutaka kutafuta namna hiyo,pengine haikupendeza machoni pa moyo kwa wale wanaotenda mbele za watu,maana huwezi kuchuna watu ngozi na kuwakata viungo ukisema tunatafuta jera,wengi wetu huwa wamekosa amani ya moyo katika kuona maisha yao,wao wanakuwa ni kama ngamia wanene kwenye tundu la sindano,fikiri ngamia kunenepa,fikiri ngamia kunawili,fikiri ngamia mtaabikaji kutoka jangwani na kuishi nji kavu..

Pengine ni hizi hali za hewa zinazobadilika kwa mara inapobadilika,ikiwa ni hali  yenyewe au hewa ikaja bila ya kuwapo hali Fulani,hapo yakaja mafuriko,tena watu wasife ila waone,ili nao wao wakajiandaa na mafuriko,ukisema kesho upigane kuna wengine hatutajiandaa vizuri na ikija vita ndiyo tutakufa vizuri,lakini uijue maana ukapigane ya nini na kama hutaki hivyo basi unenepe ukiwa umeridhishwa na matakwa yako na asikuchagulie mtu unene,wako ndiyo mti mwema kwani ukiumwagilia vyema ndiyo uwingi wa matunda katika kuujaza mti.

Hakuna mtu anayekatazwa kuridhika,hakuna mtu anayekatazwa kunenepa hakuna mtu aliyesema kuwa mwembamba ni bora,kama na endapo lako limeonekana basi timizia haja,liweke likiwa limetendeka endapo kuna mapenzi nayo,hapo ikiwa chaguo limehusika,pengine ukataka sio chaguzi lako na usishangae ukikonda,usishangae kuona tofauti ya vile ndivyo,ndivyo ndiyo vile ya vile itakiwavyo yaani kwa mtu ikaleta kuridhika ikiwa imetarajiwa hivyo,furaha mtu hakupi bila yake,yako ni njema ya kuwa si ya mtu,hapa ukaridhika ya kuwa raha tunajipa wenyewe,raha ni lazima kuisubiri,raha zipo nyingi ni kusema ipi ni bora na mwingine akasikia ikiwa mwengine haijui shida,Yule wa mwisho atatenda tu tena ikiwa ni kwa kusubiria akitaka kunenepa.

Kumbe pengine hatutaki kunenepa zaidi ya  kubadilika,hapa unahitaji mabadiliko kama ulikuwa unapigana basi usipigane,kama ulikuwa hupigani basi usipigane,maana kwa mazuri huja baada ya mabadiliko,kubadilika ni kwenda na muda kama vile giza linavyokwenda na nyakati zake,likatoka na usiku kuwa mnene,usiku ni mwembamba yasemekana maana hilo nene lisingetokea,hapa tutabadilika hata kwa lazima,maana maisha ndiyo yanasema hivyo,kama kuna waliosikia basi na wengine watende ila uangalie usitake kunenepa kwa kutamani,maana matamanio nayo huja kimabadiliko,yenyewe huwa yanaenda na siku tunaita fashion,kumbe nyengine mbwembwe tu kiachohitajika ni kwenda na fashion.

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...