Friday, February 3, 2012

TUNAWAZA KUKOSA,TUSIPOJUA NI VIPI TUMEPATA..


Mawazo ni sehemu ya maisha ya mwanadamu,katika kupitia na kufanya vile au kile ilivyotakiwa.Kuna mengi ambayo mwanadamu anaweza kuwaza ikiwa  ya furaha,kejeli,chuki,upweke,na ya ki kawaida kabisa,mawazo huweza kurudisha na kukamilisha mipango au malengo ya mwanadamu ikiwa sahihi pale anapokuwa na utambuzi zaidi.

Kweli inapasa utofauti,ikiwa wengine wako kawaida basi na sisi tuwe,ili ikaonekane tofauti kwa wengin,labda tuseme tumepata ikiwa ni mvuto wa kupata na vingine,vile ambavyo yeyote yule anavyo kwa miliki ya uhalisia wowote,ikawe na maana ya maamuzi kwani yeyote anayeishi anayo mawazo,katika yote na hata yale asiyoyaomba,juzi hapa tulifanikiwa kama mvua isingeendelea kunyesha,kumbe hatukufanikiwa ila ilipasa kwa mwelekeo wa mienendo na shughuri zilizokuwa zikifanywa ziliashiria jambo,ikiwa kila mwanaadamu anaukaribu na yaliyobora yake,na sio kwamba tulifeli sasa,labda tumefauru tofauti,mda mwingine uhakika tunakuwa hatuna ni kwa sababu mengine mambo yanakuwa ni ya wengine,hatutaweza kuyafuatilia ya wenzetu na yetu tumeyaacha chumbani,hapa tutajiongezea mawazo,labda tuseme tumeweza kuyafuatilia ya wenzetu na yetu tumeyaacha chumbani,haya mengi sana yamechanganyika na ya watu..na hii ndio hufanya kushindwa,au hata kufauru ikiwa lengo,asiyependa upumbavu ndiyo yule anayetaka maana,kile kinachoingia hakiingii hivi hivi ni lazima kiwe na njia,na kama walisema tusikie na tukaziba masikio yetu basi hatutaelewa vizuri kwani yaliyosikika si yale yaliyoonekana mdomoni.

Katika kufanya ni kunatokea na kile unachokitaka kitokee,kama hatutajua ni namna gani tumevifanya basi hata tunapovipata tusiseme ni sisi tumefanya,maana wapo waliofanya ndio wakasema tugawane,kwa yule aliyegawa..ikiwa anaye gawa anagawa chochote kilichomzidia,ikiwa tumemwita mwenzetu mmoja na kibri ni lazima tuelewe kimetoka wapi,isije ikawa ni chetu maana chuki hugawika kwa upendo,tukawapa wengine wasiwe na hatia na kwa uzito tu ikawe kujibu kwa mitetemo,yule akaonekana muongo kwa kutetemeka,tuache kufanya kufahamu herufi kabla ya maneno,maana hayo yakiunganika yatatuangamiza zaidi.mwanadamu amependa basi amepata ikiwa alitafuta,tutafikiria yaliyo sahihi na mabovu yataendelea kuharibika,kwani malengo yapo,na nani anaweza kuyafuatilia,kwa kutokujua idadi maana tungesema ni mengi,au machache endapo yangehesabika,hivyi vyote hata ikawa hakuna lolote yaani hakuna cha kuhesabu hata vingi vikawa idadi,mwanzo ukigundulika mwishowe hueleweka,mtu anaposema pole sio kaumia yeye,

Yale yaliyopatikana sasa ndio yaliyokosekana mwanzo,yakiwa na ukosekanaji pale palipo na uhitaji,haya mengi sio ya kuyasumbukia labda iwe imeeleweka hayo ni mengi kiasi gani,tutasaidiana sana lakini tutafikia tofauti ikiwa usaidizi mwingine haufanyiki baada ya kusikilizwa,na ndio baadae tusiseme yale ni ya Fulani na haya ni ya nani,vichwa vitauma endapo dawa zitaonekana,maana bila hivyo tena wanaadamu watahitaji kula nyama ya  mwanadamu mwenzao,tunaweza tengeneza njia ya msitu wa miba,,haiwezi kuonekana njia ikiwa wale wengine walikataa kusikia,hatutaweza kuyafikia ikiwa tu tumekaa na kushindwa kutembea,yule anaye tembea anajua mengi,maana atakuja hata nyumbani akikwambia ana njaa,njaa haijatokana na kazi za huko ya kuwa mwanadamu ni lazima ale.labda iwe na awe ameelelewa hivyo.

Yawepo,yasiwepo yatatafutwa.
Lengo ni kuyapata!!

By:Benson G.Makaya,
Tel:+255714336657.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...