Tuesday, July 31, 2012

MAKOSA..


Machache yanakuwa ni ya kila mtu zaidi ya mwengine aliyonayo,maana kuna kusikia ikiwa mmoja amefanya tofauti,namna ya kusema ilivyo na kufanya huwa mbaya zaidi ya watu vile wanavyosema,ikiwa kiti cha mtu mmoja ni makosa kukaliwa na watu wawili,hapo baadaye tukaja na kuambiana ilibidi kufanya hivyo baada ya maongezi,na bila kudhani kabla mapema kama maongezi hayakuwepo.kumbe siyo lazima mmoja kuona vile walivyoona wengine,hata katika upande wako jua hayo ni ya kwako tu.

Ni makosa sana kumfundisha mtoto maswala ya kikubwa,ni makosa sana hata kumwona mtoto akifanya mambo ya kikubwa,pengine hapa tumeshindwa kuambiana ya kitoto ni yapi,na ya kikubwa ni yapi.pengine na watu hao wakafahamike bila ya heshima ya umri maana na yenyewe imeleta ukubwa,kuna wakubwa wanamambo ya kitoto na hayo ni makosa makubwa,pengine kwa upande wangu,labda na watoto waachwe watende makubwa.

Inasemeka katika makosa ni namna ya kuweza kufanikiwa,na wanofanikiwa ni wote ikiwa ni watoto na wakubwa,mafanikio hayana umri,pengine ndiyo maana mwanadamu anaweza kufanikiwa katika umri wowote,hii ikiwa kama atachelewa sana basi kuna makosa aliyafanya,pengine ni mipango tu.makosa sio ya kumfaya mtu kukata tamaa ya maisha kwani ndiyo nguzo ya kufanikiwa,hata mwanadamu asifanikiwe bila makosa,tunaweza kukosa vingi ikiwa ni pamoja na pesa,afya na yetu mahitaji mengineyo.tukubari kukosa pale inapotokea ikiwa ni nafasi pekee katika kuelekea kufanikiwa,lakini pale tunapojifunza kweli.

MACHONI..


Machoni kama watu mwishoni hawana utu..hawa si watu kabisa alisemeka hadi moyoni,hawa si watu kabisa kabisa.maana yawezekana na sisi tumezoea sana kupewa kwa nyuma,tunataka tunapotenda wema basi turudishiwe na wema,hawa watu wa machoni sio wa mafichoni ndiyo maana kuna kuonana,pengine hata kuonekana na kusikika.tenda wema achana na ya mwengine na tembea zako,pengine ikiwa imekulazimu kutokea isije kuwa imeilazimu ikutokee,sijui utaonekana wa namna gani machoni pa watu.

Umepewa kijiti peleka mbele unarudisha nyuma kufanya nini?tuachane na story za kuonekana machoni wachache wakilia moyoni,hili halitakuwa la mmoja lakini kwa kila Yule moyoni litakayemuingilia.tena ikiwa kwa vurugu maana hata moyo unaona katika namna yake,pengine ndiyo maana tunachagua ya kufanya,yupi mbaya aliyeamua kufanya mabaya au moyo wa uliyeamua kufanya mabaya?maana pengine kila mmoja wapo angejua angefanya mabaya tu.

Karibu tusogeleane maana tusikie mioyo inavyodunda,asante mama karibu yako mikono kuitizamia presha,sijui zitakuwa ni homa au maralia za taifa,kwa macho hatutaona tukisubiri hatuonani,tenda unaloliona ukisubiri usimsingizie shetani,kama ilivyo kutokutenda ni ‘kutenda’kwani kinachofanyika hapo ni maamuzi,nafsi ya mtu ndiyo inaamua.hivyo tokea machoni mpaka katika nafsi ya mtu hapo ni kasi sana,maana tunasema haya mengine tumuachie maulana.nafsi,moyo,utu vimebebwa na kitu machoni

MTAZAMO..


Naona ubadirishe namna ya kutawala pengine unaowatawala wakaelewa wanatawaliwa na nini,pengine nani maana haina haja ya kusemea gizani.nilipotizama baadhi ya matendo yake nilishtuka kwa kuona,ni kweli maovu kwa kujua mema unayotizamia wewe,pengine mimi ni wewe lakini siwezi kuwa wewe,maana inahitajika wewe kuwa mwenyewe,kwa mtazamo wangu ni kheri kila mtu akafikiria lake maana maswali yanakuja kutupa majibu ya ulipotizamia.

Ningejenga barabara mbili za juu na chini,hizo zipo sawa kwa mtizamo wangu ni kheri ungekamilisha hizi za chini kwanza,hapa si unajua unachokifanya sio kugombeza kwa mtazamo wangu ni kueleza,kwa maana pengine watasema ‘alisema’. Sisi tumepita lakini wao wanokuja patachimbika sasa ni vizazi vinavyotembea na tufikiri unapotafuta unamtafutia nani kwa  maisha ya mtanzania sio ya kulala njaa labda uwe umeathirika kimanzingira.

Hivi kesho nitajali zaidi mtazamo wangu kwa kuwa na wako tofauti,basi fikiri kutenda ukizubaa subiri kalenda,maana ya kuyaona hayaeleweki ya mwengine kuliko yako,yasiyoeleweka kusemeka kueleweka,watu na wenyewe hawaelewi mitazamo yao wanachotaka ni kile walichokuwa nacho chao.pengine jumapili njema  ni ile ya kuisemea jana,pengine tukiwa na mapenzi huku tukimsujudu maulana.namshukuru baba kwa hiyo mitazamo ya maana.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...