Machoni kama watu mwishoni hawana utu..hawa si watu kabisa
alisemeka hadi moyoni,hawa si watu kabisa kabisa.maana yawezekana
na sisi tumezoea sana kupewa kwa nyuma,tunataka tunapotenda wema basi
turudishiwe na wema,hawa watu wa machoni sio wa mafichoni ndiyo maana kuna
kuonana,pengine hata kuonekana na kusikika.tenda wema achana na ya mwengine na
tembea zako,pengine ikiwa imekulazimu kutokea isije kuwa imeilazimu
ikutokee,sijui utaonekana wa namna gani machoni pa watu.
Umepewa kijiti peleka mbele unarudisha nyuma kufanya
nini?tuachane na story za kuonekana machoni wachache wakilia moyoni,hili
halitakuwa la mmoja lakini kwa kila Yule moyoni litakayemuingilia.tena ikiwa
kwa vurugu maana hata moyo unaona katika namna yake,pengine ndiyo maana
tunachagua ya kufanya,yupi mbaya aliyeamua kufanya mabaya au moyo wa uliyeamua
kufanya mabaya?maana pengine kila mmoja wapo angejua angefanya mabaya tu.
Karibu tusogeleane maana tusikie mioyo inavyodunda,asante
mama karibu yako mikono kuitizamia presha,sijui zitakuwa ni homa au maralia za
taifa,kwa macho hatutaona tukisubiri hatuonani,tenda unaloliona ukisubiri
usimsingizie shetani,kama ilivyo kutokutenda ni ‘kutenda’kwani kinachofanyika
hapo ni maamuzi,nafsi ya mtu ndiyo inaamua.hivyo tokea machoni mpaka katika
nafsi ya mtu hapo ni kasi sana,maana tunasema haya mengine tumuachie maulana.nafsi,moyo,utu vimebebwa na kitu machoni
No comments:
Post a Comment