Friday, November 2, 2012

NISHIKE..


Utawaza kushika maneno ya bwana mungu kwa kuwa yapo katika maandishi na kujifanya kujua kusoma,maana ni wazi kama angekuwa mbuzi sababu zingepigiwa mstari kwa kuwa ni sahihi,pengine ili kutokupigiwa mstari tukae ukinishika mkono kwa kunielekeza,maana pengine naona giza,huo mwanga siyo kama huu,huo nahitaji kushika kwa kunipendezesha,acha harufu kwani umepuliza wa kutosha sasa angarau nikaotee jua,najua japo nikishika moto pengine nitaotea kwa yale mema kuwa mabaya,kwa ule wema kuwa wa mbaya.

Ukishika bilioni lazima utakuwa billionea,ukishika maneno ya bwana mungu wako lazima utakuwa mtoto wa mungu wako,pengine ikiwa umeyashika kwa sababu ipi,ikiwa umeyashika unayoyajua wewe,kesho mwanafunzi anapofeli darasani aulizwe nini anataka ili afauru,pengine isipokuwa kwa kushika ramani ama kuleta amani.maana ikiwa umefeli umetaka kushitaki,haina maana kwa waliofauru kwa kutokwenda kushitaki.

Hapa kunaweza kuwa na chaguzi hasa zaidi katika yale mazuri na mabaya,yale ambayo mmoja akayaona kuwa ndiyo na mwengine akasema  kwa mshituko kwamba siyo,kuwa na imani kwa lolote lile unalohitaji kulishika,imani ya kushika unapohitaji siyo ya kuthubutu endapo kukiwa na mahitaji,tabu zikamfanye mtu ajitambue zaidi yakuwa ameshika yale yaliyomletea taabu ama raha zaidi.ama tuyashike yale tuliyofundishwa zaidi.

SAHAU.


Kuna muda yapasa kujifanya kutokujua kwa kusahau pengine ikiwa ni makusudi ama vile ikawe ni mpango wako mwenyewe,kama ungejulishwa lile lililo katika ndoto zako ndiyo ukweli hakika ungeamini yako,sasa unaweza kuwa umesahau,muda huu unaweza ukawa kama siyo yale uliyokuwa unayaota kwa kuwa ni haki ukweli upo,pengine ukiwa unaamini yako kwa kuwa ndoto hazikusema,ama zimesema lakini umesahau kwani mambo na yenyewe ni mengi mno kwa kujichanganya na nafsi.

Utasikia huyu mimi simpendi,hapo akiwa ameshindwa yeye kukupenda,ikapita dakika kwa yanayofahamika ni lazima kuwa wazi,maana pengine unaweza kutega kwa kusahau,ukijiuliza umesahau yapi kama siyo unayoyajua,maana mapya na yenyewe yanapokuja huleta utofauti na yale ya mwanzo,hawa wa kwanza wakiwa wamekula sana,ikiwa siyo wa kwanza kabisa wao hawakula na wakijifanya wamesahau,na kwa muda unavyokwenda hawa waliokuwa hawajui imekuja kujua,maana kujitambua.

Kesho sahau sema jana nilisahau,usisubiri kukumbushwa maana wengine wanakusahaulisha kwa lazima,wakitaka kukamilisha kauli ile ya kutokupenda mengine yamekuja baada ya wengine nao kuota tofauti,wakiamini kusherehekea ndoto za wenzao kuliko yale ya kwao,unaweza tangaza vita kwa kupotelewa na siraha  bila ya kujua kama ulikuwa hujui matumizi yake,nisisahau mimi Siraha,Nisisahau mimi siku za vitani.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...