Kuna muda yapasa kujifanya kutokujua kwa kusahau pengine ikiwa ni makusudi ama vile ikawe ni mpango wako mwenyewe,kama ungejulishwa lile lililo katika ndoto zako ndiyo ukweli hakika ungeamini yako,sasa unaweza kuwa umesahau,muda huu unaweza ukawa kama siyo yale uliyokuwa unayaota kwa kuwa ni haki ukweli upo,pengine ukiwa unaamini yako kwa kuwa ndoto hazikusema,ama zimesema lakini umesahau kwani mambo na yenyewe ni mengi mno kwa kujichanganya na nafsi.
Utasikia huyu mimi simpendi,hapo akiwa ameshindwa yeye kukupenda,ikapita dakika kwa yanayofahamika ni lazima kuwa wazi,maana pengine unaweza kutega kwa kusahau,ukijiuliza umesahau yapi kama siyo unayoyajua,maana mapya na yenyewe yanapokuja huleta utofauti na yale ya mwanzo,hawa wa kwanza wakiwa wamekula sana,ikiwa siyo wa kwanza kabisa wao hawakula na wakijifanya wamesahau,na kwa muda unavyokwenda hawa waliokuwa hawajui imekuja kujua,maana kujitambua.
Kesho sahau sema jana nilisahau,usisubiri kukumbushwa maana wengine wanakusahaulisha kwa lazima,wakitaka kukamilisha kauli ile ya kutokupenda mengine yamekuja baada ya wengine nao kuota tofauti,wakiamini kusherehekea ndoto za wenzao kuliko yale ya kwao,unaweza tangaza vita kwa kupotelewa na siraha bila ya kujua kama ulikuwa hujui matumizi yake,nisisahau mimi Siraha,Nisisahau mimi siku za vitani.
No comments:
Post a Comment