Saturday, May 5, 2012

MATEMBEZI


tuwaze vile vinavyofanya kutembea na sio vile vinavyofanya kutembea kutembeza
sio kwa ubinadamu tutafikiri labda ni kwa kupanga maneno,
ikiwa kwa moja iliyokubwa ndiyo huwa mwongozo,
katika kuongoza hapa kuna mbinu tofauti pengine kwa walio na hitaji la kupigana vita ya kuwa si matusi zaidi ya kumfanya mtu kuelewa,
maana wewe ndiyo unakuwa mwalimu,au mpiganaji..
pengine mwalimu hajui zaidi ya mpiganaji
hapa tutafikiri maana,

pengine ni kurejesha viumbe duniani ikiwa tunasema tutazaliwa mara ya pili maana ingalikuwa ni zamu ya mtu wa mwaka mwingine basi tungekuwa tunachelewa sana,
ikifahamika kwa wengine mwisho wa dunia ulishatakiwa kufika,
hapa kuamini,
ikiwa lengo ni kutaka kweli kutembeza,
pengine tusijari mwendo zaidi ya kufika,
maana kama itaeleweka safari ulianza zamani basi kuna uwalakini wa kuitwa na mwenfo pole,
maana tukijaribu kupunguza kasi ya maneno hapo tutakuwa tunapunguza uwingi,bora yakawe maneno yote na huo upole pia,
simba haelekezwi na swala kumkamata twiga,
bali ukaribu wa simba na swala ni zaidi ya vile wa twiga,
maana twiga yaweza kuwa ni mtamu au basi yu mrembo na urefu wake na ikawe nyama ya baadaye,
wale twiga wafupi ndiyo wale warefu wa wenzao.

tutatengeneza vingi na tukajua ni vile vile,
wazee wa zamani wanafikra ya kuwa na uzoefu wa maisha
kijana wa sasa anatakiwa awe na fikra ili kuweza kupingana na shindo za maisha,
hapa fikra ipi sasa huwa ya kijana na mzee,
na hapa ndiyo maana na kuweza kifikiri,
yaani isingelikuwa hivi basi siyo maana ya kuwa vile maana sio lazima,,
pale mtu atakuwa na fikra,
pengine imani,
ieleweke sio dini,
kwani hata tukaulizwa dini ni nini tutasema ni imani bila ya kuifahamu imani yenyewe,
pengine sisi hizo sio dini zetu,
ni imani zetu...
pengine sisi ni imani zetu na wengine sio dini zao,..

hapa ni kuwa mahala kote maana unaweza kutokuelewa bila kufikiri,
yaani hamsini hamsini,bila ya kumalizia na mia
maana hilo ni jibu baada ya kutembea
yule anayetumia imani kufikiri ni baada ya ubongo,
maana ubongo ni kuwasilisha..
basi tukafikiri kutengeneza roboti bila ya kujua tutawaundia nini,
maana hata tusiwaze kutembeza,,
si watakuwa kidogo kidogo..
watatubeba wale..

imefika wakati tunataka kutembeza vile visivyotembezeka,
maana kama utamtembeza mtoto mchanga ni sawa na kutembeza roboti la umeme kwa nguvu,
hapo nguvu imesema.
tena kama ni umeme unatembeza si nyepesi kwa mwanadamu kutembeza,
maana si tungetembeza!!
hapa tusimfikirie mungu sana labda kila mtu awe na fikra zake,
hii itasaidia sana katika kutembeza maisha,,
pengine maisha hatujayafikiria sisi tu,
walivyoanza wazee sidhani kama tuliwauliza japo hata kuwasikia wakisema,
kama walikuwa wakimya jaribu kujiuliza maana ndiyo kukua na maswali,
ili kuweza mtihani inakuwa vyema kwa kujiandaaa,
tutajiandaaje bila maswali?

kweli yapasa tujipe maswali,
tena mengine tuwasaidie na wengine,
pale tu tunalipolizika na maksi zetu
ikiwa na mshindo basi tutembee tuyaone kwani macho hayasemi mma..

By:Benson G.Makaya

HALISIA.


Zote ni namna za kuweza kuwa halisi nikimaanisha unaweza kuwa katika namna nyingi,kuwa halisi ni kuwa wewe,ni kuwepo na vile vinavyotakiwa,
ninaposema halisi simaanishi ilivyo kama neno lenyewe,halisi katika mazungumzo huleta picha nzuri,maana wengi watataka kujua hapo,hapo ni  nini maana yake halisi,
tena bila kusahau  kwa kuwa unajiona upo juu ama chini,usijisahau kwa namna yoyote uliyonayo,
maana hapo unataka uhalisia,ikiwa ni chakula kina mapishi,na wala si matamshi kwa yule msemaji.

katika namna iliyo moja ni lazima kuufahamu uhalisia maana unaweza kunenepa kwa vitambi na kujisifia kuwa umeweza,tena utakuwa umeweza kweli kama uhalisia ilikuwa ni kutafuta hilo,
labda unene halisi ni mzuri,pengine haina haja ya mazoezi kwani sio halisi,
yenyewe huleta namna nyingine yenye uhalisia wake,

Kwa jicho dogo kuona sio kuona kidogo,kwa macho makubwa kuona sio kuona kikubwa,akionacho mtu ni kile anachokifanya,uhalisia haulazimishwi ,
siwezi kuwa mtumwa halisi,naweza kuwa mfanyabiashara halisi,
siwezi kuwa mfanyakazi halisi,hapa sijui uhalisia wetu uko wapi,
maana wangu ndiyo ninaoufanya.pengine katika nafsi toa uhalisia wako na itakusaidia maishani mwako.

Katika maisha  kuwa halisi ni kuishi kiuhalisia pengine halisi inatafutwa,halisi katika namna yoyote inavyoweza kuwa kwa mmoja kutokupenda siyo halisi ya mwingine,maana bila kuwepo usingepata picha,ikipatikana ya tatu basi ya kwanza ilikuwepo,ndiyo idadi zikaja ili kuleta namba halisi,
ikiwapo moja yenyewe yapasa kuitafuta na mbili,
maana inahitajika uhalisia katika kuhesabu pale tu unapothubutu kuutaka uhalisia wako

muda ungekuwa hauendi nigebaki kuwa vile,kubaki. maana nimetoka pale nyuma ama mbele kuelekea katika namna nyingine ambayo nyingine hiyo ndiyo inatenganisha na kuleta uhalisia,
ikiwa lengo liwe  ndiyo ama sio kuutafuta,hata ikawe lakini lengo ni la mtu,
Siwezi kuwa na lengo moja na kufanya kimoja,
hapa ikiwa mmoja yupo na mwingine,

Pale awepo mwingine ni kwa sababu unataka kujua namna ya uhalisia wa kwanza,
tena ukauona maana pengine ni ule wa nyuma,kama ilivyo halisi ya umoja na utofauti wa hasi yake,
kuwa hasi sio chanya hiyo ni halisi,kumbe hata halisi sio nzuri kwa wakati mpya,
kujua jambo si mwisho ukitafuta wanaojua lazima walikuwa hawajui,
na huo ndiyo ulikuwa uhalisia wao,pengine unapofanya na kuona hayaishi ujue ndiyo halisi yenyewe,
kama ulizoea kuvaa rubega sasa ni nguo za pamba na mengineyo ya halisi yake
pengine uhalisia unakuja kwa yale ya asili,
kama mwanzo vile,

yapi mema mpaka mtu ukatamani kurudi na kuwa mtoto?
hapa unatamani asili,maana ulivyokuwa na asili haukuufahamu uhalisia,
kumbe uhalisia unatembea tofauti na asili

Benson G.Makaya

SAHIHI...


Sahihi ni namna,sahihi ni kitu,sahihi ni uwezo,sahihi ni hali,sahihi ni neno linaloleta maana.
yaweza kuwa maana ipo lakini ikawa sio sahihi,ili isiwe sio sahihi yapasa kusahihishika,
ingawa na yenyewe ni maana,wanaosahihishika sio wakosaji,
ni wale wanaotaka kusahihisha,pengine wanafanya sahihi,au wameona sahihi au hata wao wakawa sahihi.

Tunapozituliza nafsi,ikiwa na kichwa kwa ujumla ni lazima kuwa sahihi,
 katika yale yaliyosemeka mwanzo,ikiwa kama ni kitu basi kieleweke kuwa sahihi,
maana ubovu nao unakuwepo na usahihi wake,ikiwa mmoja akafikiri sahihi zaidi ya mwingine kwa upande ulio wake,sahihi huja katika matokeo ya maswali ya kuwa  maswali huwa sahihi,
pengine tukikaa kimya tunakuwa tunafikiria lakini sio sahihi zaidi ya swali linapokuja kama unafikiria nini,
 pengine tuingie ndani zaidi,ikiwa tumetaka kuujua usahihi.

Siyo usahihi wa makosa wakati bado hatujafa,maana mengine bado hayajatendeka,
 kama mtu kalenga kukosea ni si vile afikiriavyo aliyepatia,
maana kama kuinama ni sahihi basi watu wengi wasingesimama,
tena tungebaki na haja zetu bila ya kuonekana ni sahihi endapo tukataka kusimama,
hapa tufanye sahihi ilivyo katika umbo na hali ndiyo usahihi wenyewe.

Usahihi sio kama swali limekuja mwanzo,kumbe bora sahihi kuliko swali,
maana kama kuna kujibu kwa wakati huu ni lazima kufikiri kuhusu usahihi,usahihi ni baada ya mtihani,
mtihani ni maswali au swali linaloweza kukupa usahihi,maswali yapo mengi sana,yote ni sahihi kwani yana majibu yake.

Katika kufikiri lile moja mengine mengi huja ndani yake,pale ndipo usahihi unapopotea,
tena siyo kupotea zaidi ni kujificha,maana kile kinachogombaniwa na wengi ndilo swali hilo,
hapo ikiwa kila mtu anataka kuweka ama kuleta usahihi wake,
yaani majibu..na baada ya majibu ndiyo huja usahihi.sahihi ya mwanzo ndiyo halisi ya mwisho na ndiyo maana kukawa na mwalimu,yeye akajua,akafikiria,akaweka..

Pengine na akadanganye kabisa lakini kwa mwanafunzi hilo ndilo jibu sahihi.Tuyaache maswali sahihi yaje maana majibu yapo mengi sana,tena tutayajibu kutokana na vile mavazi yetu sahihi yalivyo,
hili ni kama swali maana usahihi unategemewa na wewe.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...