Wednesday, August 15, 2012

MZAO..


Omba kuzaliwa lakini sio kuzaa,pengine ni wazi inahitajika kwa umri fulani kupata japo mwana,lakini ni lazima tuangalie na kizazi kilichopo,maana kama wangu angekuwa amechelewa kidogo basi ningemuombea uhamisho wa kuzaliwa mbele kidogo,kwa maana kwangu haikuwa bado.unaposikia bilabila ni ya hakuna,sasa kama vizazi vipo na inasemekana kuwa hicho kizazi kijacho kitakuwa na hasara sana,ningependa kufahamu hatari yake lakini kumbe ni ile ile namna ya kutaka kutokufanya,maana hichi kilichotabiriwa kuwa kibovu kimekuwa kizima ni kwa sababu wale wazima walikuwa wakifikiria hasara.

Ikiwa mnyama anahitaji kupata mzao mzuri ni lazima awe anakula vizuri na kuudhulia maswala ya afya,pengine wazee wa zamani ni wazi walikuwa ni watu wa ajabu sana,sishangai ngozi nyeusi kuitwa nyani,kwani unapochelewa kuingia shuleni ni viboko na wala hatuwezi kusema wewe sio mwanafunzi,kwani hata pengine baadaye itakuja na kuulizana ‘una mtoto gani,ama vile ana umri gani?’hapo ikisahaulika kama walishamfukuza darasani kwa kuchelewa.na baadaye yakitakiwa majibu kupitia kile kilichokifanyika

Hakuna mzao mbaya bila ya mtu kutokulitumikisha tumbo lake,pengine inapaswa hadi kulala lala chini ali mradi  usisikike..kama nyoka vile.maana kwa muda uliopo sio lazima ya kusema kwamba bora angetangulia fulani,maana hii au hawa wa leo wamekuja leta ubovu,hapa nikikumbuka ya kwamba mti haupewi lawama bila ya jua,maana hata lisipokuwepo litasinyaa tu,pengine ikiwa ni mzao wa mti mwema

NAMNA(2).

Katika kufanya ni kufanya yale yanayoendana na kile kinachoendana na maisha yako,ikiwa maisha yanahitaji uvumilivu wa maelfu ya muda,kuna namna ya vile unaweza kujiuliza ni namna gani unaweza kufanya  maisha yako yakaonekana na mtazamo bora ikiwa yameonekana yanatakiwa kurekebishwa,pengine ni katika mapenzi ama vile ilivyo katika hali ya kuuboresha mwili,wachache wakiwa wanafaidi kwa migongo ya wengi,na hii ikiwa wengi wetu ni hatujitambui,ingawa kila siku tunazungumza maswala ya kujitambua na bila ya kuelewa ni kujitambua katika namna ipi?

Leo imefika usikubari kuwa mzigo,pengine ikiwa utabebwa sana tena vibaya maana na mbebaji akiwa amechoka yu radhi kuutupa mzigo wenyewe,ikiwa hakuna namna ya kuweza kusema maisha ni marahisi kwa sasa,basi ni kuyapokea kwa utambuzi  wa kufanya  na kupokea kile ambacho mtu amekiamua kupitia fikra zake mwenyewe,pengine ukawa  hausikilizani kwa sababu ya kufanya kwako ni tofauti tena bila ya kujua unaweza kutoa lawama,na bila kujilaumu mwenyewe.

Hakuna Yule asiye na kitu,maana hata katika mawazo,swala ni utofauti ambao kila mtu anajitahidi katika kufikisha maisha yake mahala husika,unapotaka kufika mahala fulani hapo ni lazima utambue mahala ulipo,ikiwa na watu zingatio wanaotakiwa kujitambua ni tofauti,kawaida ya malengo huja baada ya kufanya yale unayoyatambua,hivyo ikaja wakati tumefanya tofauti hiyo ni namna ya kujitambua tofauti,pengine hata   mtu ukafanya ukaeleweka kufanya tofauti na jinsi ilivyo.

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...