Hata zikiwa nyingi wachache hutaka moja tu kauli kuielewa,kwa kujua kwa
yale mengi hakuna wa kuyaweza naye.ukisikia kauli lazima uishike isiwe
kauli nyingine zikasahaulika,ama
ikaonekana vile walivyosema wengine,kwamba kauli ya mtoto kumwambia mkubwa yaweza
kuwa makosa ki heshima,lakini siyo ikawe mkubwa kwa mkubwa
mwenzake,ikawa si hekima,maana itaoneka dhambi kwa kujaribu kuyafanya ya juani wakati kauli
nyingine ni za gizani.
Ni wazi hakuna lililo sahihi zaidi yako Mungu,kwa Yule
anayebisha ni sawa na kufananisha ndiyo na hapana ,ukikaa na kukuwa bila
kuelewa utanawa sana kichwa kwa kupata moto tena hutaelewa nini cha kufanya pengine ukiwa haujafanya kitu hapo mwanzo lakini kauli zako zikakukuponza.
Ninatoa kauli yangu pale inaponibidi ikiwa nazijua haki zangu,akili yangu inajua cha ziada nje ya mwili kinachoendelea,hivyo kauli yako yaweza kukuliza ikiwa hujachukua dhamna ya kuyabeba majibu yatokanayo na kauli zako,ni mizigo ya ndani,wachache wanafunzi huelewa nini mwalimu anachofundisha,maana kila
mwanafunzi anaelewa yake pale inapokuwa nafasi na wakati wa kila mmoja kutoa kauli yake katika uelewa
Ni kweli kauli nyingine
ni makosa sana kutamkwa,si vyema kusema kitu usichokifahamu na kugeuza kauli yako ya kweli,ni wazi hata samahani isimaanishe kitu hata ikawe kwa mtu
kuuana na mwenziwe.kauli nyingine hazitakiwi kukumbukwa,kauli nyingine zina
maana ya kuleta kauli nyingine zisizo na maana.Chunga kauli.