Katika malengo yanayomfanya mwanadamu kuweza kuishi pengine
ikiwa ni kwa muda fulani ama ki namna ilivyo kwa mtu akataka furaha iliyoje ndani
ya maisha yake,na ikiwa mwanadamu unaishi na hutaki furaha kuna ulazima wa
kuonekana kutokukamilika,kwani hata mahitaji pengine yasiwe yako,ikiwa tunapokutana tunafundi shana,leo ikaja zamu yako kwa kutokueleweshana na kesho
akaja mwanafunzi ili kumuelekeza,furaha
haipimwi na mizani labda wanene wakawa na roho kubwa,ingawa maisha yako ni kile
unachokifanya,kile kinachoonekana katika biashara yako,kazi zako ndiyo mtazamo
wa maisha yako.
Unaweza kuwa na maana kubwa katika lile ulifanyalo,ikiwa
hakuna kile kinachoweza kukamalika bila kujitoa/nguvu,kutoa nguvu inapasa
kufanya kila mara,ikiwa kama mazoezi,mtu akaogopa kufanya lile lake kwa kuhofia
mengine kwani unaweza ukawa unaishi maisha ya mwenzako,kila mshindi hushinda kwa
kuonyesha njia,kila mshindwa hushindwa kwakuonyesha njia pengine ile ile,kila
mtu anawakilisha zawadi ile aliyopewa na mwenyezi mungu,kwa kupita katika majaribu,kulia,kucheka ,kuchekesha hata
kunyamazisha,hayo yote yakiwa ni madhumuni ya maisha yako,kusaidia watu na kusaidiwa hii ieleweke kuwa ndiyo njia ya kupumua,ni njia ya
kufikiri..njia ya kuishi,maana bila hivyo haikuwa na maana ya kuishi katika
dunia ya furaha.
Inapasa kujua wapi ulipo katika maisha yako,furaha yako
umeibeba mwenyewe,kila mtu anapaswa kufanya jambo ambalo kimsingi litapelekea
mapenzi,na hii ikiwa inatupasa kuwapenda hata maadui zetu,unaweza usimchukie
mtu lakini yeye akakuchukia,ikiwa kuna watu ndiyo wametufikisha hapa tulipo,kwa
mapenzi ama uadui,maisha hayana uadui,wewe ndiyo adui wa maisha yako,wewe ndiyo
mbaya wa maisha yako,kinachobadilisha mabaya kuwa mazuri ni matumizi na muda wake,ikiwa kama mvumilivu hula mbivu,na
siye vumilia si kwamba atakula mbichi,maana na furaha haipimwi kwa kilo.
No comments:
Post a Comment