Ni kupambana,ni kutia mkazo ili jema la mtu
likaja upande wake,maana lako ni lako,maana wewe ni mtu maalum,ikiwa kuna wakati unaotofautisha maana na kuleta tafsiri
tofauti,ukiwa unaishi fanya lile la kesho maana leo imeshatokea pengine ndiyo
maana yapasa kujiandaa kabla ya safari,ikiwa kungalikuwa na uwezo wa
kutokusafiri kwa kutumia muda basi wengi wasingechelewa,haina maana ya kupita
mkato ama njia ndefu ili kuleta neno maisha,ya leo ukiyaacha utafahamu vyema
kuhusu kesho,kivingine ikawa ni ufunuo,hakuna mkato katika maisha kwani kila
mtu yapasa aishi yake.
Ikiwa kuna kufananisha
ndiyo kumeleta vitu na utofauti,ukitaka kuachia njia yako jaribu
kukalili ulipoishia,maana unaweza ukawa hauelewi na kujikuta umeelewa vyema
sana kwa kuwa ndiyo njia uliyotaka kupita,unaweza kurudia jambo mara nyingi na
usijue ni kwasababu gani haujaweza fanya lingine,hayo yakiwa ni matendo katika
maisha yako,jaribu kufikiri nini unataka,chukua hatua na jaribu kupata na
kuyaelewa ya nyuma,sisi wote tuna namna moja ya kuishi,ikiwa unaweza
kulichukulia jambo kiuhakika katika mlengo wako wowote,upe muda na njia zilizo
sahihi,hata ikiwa haujafahamu nini usahihi wake lakini muda utakuonyesha
njia,maana utafanya lile linalokusudiwa na muda.
Kama ukienda na kufikiria kila maisha ya mtu mmoja unaweza
usione mafanikio maana ni lazima ujue nini unachohitaji katika muda
sahihi,pengine yaweza kuwa tumbo linauma kwa sababu ya njaa,fikiri kama unaijua
njaa kihalisia,maana hata ikawa gari bila mafuta ni sawa na kumpa baiskeli mtoto
asiyeweza kutembea,yote yanawezekana,ikiwa unaweza kukubali kwa yale
yanayokupitia maishani mwako.hakuna mkato katika kupika nyama bila maji maana
utakuwa unachoma,jambo ni kujua.
No comments:
Post a Comment