Sunday, June 10, 2012

MUHASISI.

Hata usitumie ubaya kwa uzuri,ama ikiwa leo imetokea ukajua haitakuja tena,pengine  ikawa ni zamu yako,ama vile ikawa sisi na mali zetu.wote ni wamoja,yote ni ya kuyangoja,pengine isiwe imekuwa vyema kwa matokeo,ama vile ikawa vyema kwa wasubiriao,hapa nnazungumza lugha ya mwanzo,mwanzo ule uliokuwa pamoja ikiwa ni kutaka kufika hapa.

Mwanzo wa kuanza ni mgumu sana,pengine hapo ukatenda yako alimladi ikaja hivyo,hata usipoteze muda,kesho ni zamu yako,ukubali kwa mema yanayotendeka mwanzoni.Ikiwa unajua kuna majonzi lakini yenyewe hayastahili kuwa ya kwanza,hapo hautajenga zaidi ya kubomoa vilivyopo,moja inapoondoka hupendelea kuja mbili,hapo ikiwa imeongezeka na hatimaye kufika nyingi zaidi kwa kutoka katika uwingi.
atakayeenda wa kwanza ashukuliwe,umeenda baba tunakushukuru,maana leo tumejua ushujaa wako,pengine yalikuwa mengi yakiwa ndani yako na hivyo kufanya wakaelewa wale watu wako.

Leo sio jana,maana ndiyo unaweza kupata taarifa za kujulishana,hapa utajulishwa taarifa njema na hata mbaya,hapa ni kwa vile kwa yule inayemuhusu,tukio hili limetuhusu wote,bila kutangaza yaliyokuwa yakifanyika,haipaswi kushangaza kwa mengine kutofika,nguvu za kuweza zilionekana mwanzo,nguvu za kujibeza zingeonekana mwanzo,mshindi mpe yule anayekuwa wa kwanza,huyo tutamwita muhasisi,yaani alikuwepo mwanzo.

 Mahala pa kwanza ni vyema kuandaliwa maana hatujui huko tunakoenda kama tutakuta wametuandalia namna gani,hapa basi tunaomba,hata kiasi cha kuona,umetufanyia vingi sana kwa wanao fahamu muhasisi,nenda kapumzike salama baba Makani familia inakuombea pamoja na sisi.


Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...