Unapokwenda
ni sawa,kwa kuwa kila siku kadri ya zinavyokwenda mwanadamu anaishi katika ile
hali ya kutokusema kwamba!!na sio haieleweki,kwani kwa wasio elewa ni lazima
kubisha na kwa yule abishaye asome,aone ili aje ahakikishe ni vigumu
kuhakikisha kitu ambacho kipo hapa yaani ni wewe ujuaye usawa wake,na sisemi
kibaya kwani sio changu.hapa unaweza kuleta ugomvi na uelewe yasiyoeleweka
yanatoka wapi?
Uwakumbuke wenye
miwani,Usielewe kwamba hawataona,elewa kwamba watahitaji kuangalia zaidi,labda
kuna muda na akili ivae miwani pia,ile kama
unazuia jua usiku.Haya ya kila siku ni
magumu kuyafuatilia,ingawa kila siku unakaa ukifuatilia mambo ili ufanikiwe
kwa kile kitakacho onekana,usione nyuma.ujaribu kule Kunako onekana, siwakatazi
wale wanaorudi nyuma na kuokota vile walivyovidondosha,au kusahau, wakitumia nguvu nyingi wakiacha mengine ya muda husika yanaendelea
Masikini
hafirisiki,maskini ni yule mtafutaji,na akakae kila
siku akitafuta bila kujali ni lisilo na muda au halieleweki,maskini anayetafuta
huelewa yote
Uelewa kuwa
yasiyoeleweka ni yale anayoyafahamu ambaye hajaelewa,
ni ruksa kubwa kuunga mtaji
kwa maskini kuliko kwa tajiri maana kwa tajiri pale itakuwa ni kuungwa,labda
iwe tajiri naye ni maskini katika
nafsi,na ili uelewe vingine vipo kwa nini,kuwe na vitu vinavyoeleweka ,uwashe
moto bila mafuta na uone kama hautachoma nyumba,hapa usije singizia ni vyanzo
vingine,maana sijui zamani walitumia nini au ni mayai haya?
Ukipanda mti na ule
mkavu tegemea,mapya yapo na isije wengine wakaitwa wao ni wa kila siku,labda
wazoefu maana na mambo yenyewe yanabadilika bila taarifa,ikiwa yanaweza kuwa
ya kisasa au ya kizamani anayeyabadilisha si wa kumdhani.maana sisi tumekuwa
hatubadiliki,yaani tupo vile vile,hivyo ndivyo wasemavyo waungwana.pengine maskini
kuwa tajiri yakuwa imeonekana maskini wengi wanatamani hivyo,tajiri hawezi
kutamani kwani ametoka huko.
Ingawaje tamaa inafanya kazi popote,labda useme itakuwa sio kila siku,maana hapa utaepuka
ubishi na wale wasio elewa wakati haya ni mambo yao.Naweza kusema yetu au
yangu pia pale yatakapo nishinda yale yangu,hata nisiposema sifai kuchekwa
kwani nani anayafahamu haya yangu?ni sawa na kumshangaa yule anayeelewa akiwa
anaomba msaada wa kueleweshwa,hata ukasema kwamba Fulani huelewi naye akakataa,
usishangae amekataa
ni kwa sababu haelewi
Mengi huyafahamu,Utakufa Maskini!!
by:Benson G.Makaya
tel:+255714336657
email:bensonsmakaya@gmail.com
No comments:
Post a Comment