Friday, November 18, 2016

SHIKA YAKO

Kamilisha mipango yako ukitilia maanani kwa kile chochote ukahitaji kufanya katika namna ya kukataa kujilaumu na kukwepa lawama,Utapatwa na mshangao kwa kuona Yale yanayotokea halisia sio kama vile ulivyofokiri, ukiwa na fikra zilizochanganyika na Mawazo ya aina nyingi yenye kujua lipi ni tusi na lipi ni shukrani.

Nashukuru sana Mwenyezi Mungu kwa Pumzi yako kwa vile utakalo wewe hutimia, nakumbuka mengi machache sio kama ya mwengine, Asante Nimekuja duniani nimekuja uwanjani pengine ni mchezo unaohitaji hasira na nikakasirike tofauti.

Watu wanaona wanachowaza wao juu ya wenzao ni sahihi zaidi, yaani mtu anaamua kumwamulia mwengine kwakuwa tu labda wametofautiana katika hali zao hasa katika uchumi wa binafsi na pengine ikawe ni tabia na kujifanya nafsi ya mtu iko mikononi mwao. 

Maisha hayana uelekezi wa moja kwa moja yakakupa kanuni ili ufanye vile na ukafanane, binadamu tumetofautiana katika hali nyingi hasa ikiwa ya kwako umeyaweza Leo mwache kesho aweze mwengine unayemwona kashindwa Leo,haina haja ya kumsemea ikiwa kinachofanyika sio kosa kwake.

Ondoa wivu na roho ya kukunja katika lile jambo aliwezalo mwengine, ikiwa hujui ni bora kuuliza na kumwacha mwandishi aende na faida zake kuliko kusemea kitu kinachokuhusu wewe na kulinganisha na utofauti wa kile anachokifanya mwengine ya kuwa binafsi huna uwezo nacho.

Leo nikiangalia baadhi ya mambo yaliyoonekana na kusema hakuna aliyekamilika katika dunia hii yenye mengi, watu tumetofautiana chaguzi mmoja akaona kibaya ni kizuri  na mwengine akaone kizuri ni kizuri hiyo yote ikiwa ni kutaka kuona mazuri na kuukataa uhalisia, au kuukubali katika namna yake. 

Uhalisia huja katika pande zote lakini binadamu uufanya uhalisia wake pale anapopendezwa nao yeye, ni kheri kukaa kimya kuliko kusema kitu ambacho hakiwezi kufutika maana na kuleta uhalisia tofauti, kwani yanapokuja mabadiliko fitina na uwongo uliokithiri unaweza kuharibu picha na mtazamo wa maisha yanayokuzunguka.

Sibishani na mtu ili akapata faida,aliyetaka kuelewa aliuliza mapema kile kinachohitajika kufanyika na kikafanyika , hakuna haja ya kulazimisha kujulikana kama unajua na wakati haujui, anayefanya jambo moja huacha kutokana na mtu mwengine karibu kufanya jambo lile lile, na aliyeamua kufanya jambo hakatazwi kwa maneno ama kwa  kile kilichofanywa,na akiacha isiwe kwa maneno maana kuna binadamu wanajua ya wenzao kuliko wenzao,wakijiweka wao bora zaidi ama tu kukuchafua kwa vile mpumbavu hachagui neno la kukusemea,

Shika yako na mwache mwengine akiendelea zake.

Tuesday, October 11, 2016

KUZA KIPAWA CHAKO NA KATAA KUSHINDWA.

Vitu vinavyokuja kirahisi mbele yetu kama zawadi inaweza kukupelekea katika sehemu nyingi chagua na kuwa na uzuri  katika kila jambo, amua kutoka ndani ya mfuko wa moyo wako na kuangalia nini unataka kufanya katika maisha yako ukitakiwa kuyandeleza maono na mawazo yako.

Usijifiche bali fanya ni lazima kufanyia kazi kipawa chako ikiwa ni nguvu na tabia ya mtu, amua kwamba utajisukuma ili kufika mahali Fulani kwa nguvu zako mwenyewe,

Nguvu ya mwanadamu ni kubwa sana Zaidi ya ufikirivyo kile ulichoamua hakuna mtu awezaye kukukataza, anza kuongeza na kuimalisha malengo yako kwani mafanikio unayachungulia unayachagua wewe mwenyewe na kipaji chako kikufikishe pale.

Kila siku yakupasa kutafuta nini njia ambayo utafika siku na watu wakuulize na washangae umefikaje pale, maisha yanaweza kuwa ni silaha kwa muda mwingine na vitu vingine watu hawafundishwi hivyo sio kila kile ufanyacho ni mafanikio  yakupasa kuwa na nguvu zaidi ya maisha yako yenyewe na namna unavyoyapima mafanikio binafsi, kubali kwamba kuna watu wanaitafuta iyo nafasi uliyonayo, 

Hakikisha unatumia siku yako vyema haijalishi ukiwa na furaha ama chukizo yakupasa kutambua kuwa ni wewe upo katika hiyo hali na nini kifanyike,ukiwa unajua unachokifanya haikupasi kuwa na maisha ya katikati inakupasa kuvuka vizuizi, usijaribu kuacha kupigana na kukata tamaa, jiamini na Pigania Maisha sio leo wala kesho Kwani umekuja kuishi.

Tambua uko katika misheni ambayo inahitaji ukamilisho wako, usijikatae kwa kukosea maana wengi waliofanikiwa wamekosea sana, utajifunza kutokana na makosa bila kujali ni makosa ya aina gani maana mwenye makosa ndiye anayetegemewa kufanikiwa, sema ndiyo kwa kila jambo linalohitaji kuendelea mbele, jaribu unapopata wewe ni lazima utambue kuwa kuna nafasi nyingine katika maisha,

Kwa kile utakacho toa ndiyo hicho utaingiza, usirudi nyuma kamwe muda wa kushindwa ulishapita,kipindi kigumu huwa kinapoteza vipaji vya watu wengi na kujikuta wakibaki wakilalama na kufanya hakuna, funguo ya kufanikiwa ni kujiamini  kujifunza na kutenda kupitia makosa hayo hayo, 

Toa sadaka yako leo  kwa ajili ya kesho nzuri inayokuja na utumie ubongo wako vizuri ili kukuendesha kuwa na furaha na mafanikio unayoyategemea.

Tuesday, September 27, 2016

YAFANYE MAPITO KUWA ELIMU.

Yafanye mapito yako kuwa nguvu inayokusukuma kwenda mbele ukitegemea kuishi ndoto zako na sio kile unachokiogopa na kuhofia,wengi hawafanyiyale wanayoyategemea zaidi ya kile kilichopo pasipo kufikiri ni kwanini mtu anajawa na msongo wa mawazo yanayokataza kuishi ndoto zako.

Labda  kwa sababu ya watu na matendo yaliyopita yanaisumbua roho yako, watu wengi wanaishi wakikimbilia wasichokijua kwa kuogopa nafsi zao kubaki nyuma na baada ya kuangalia wanajikuta walichokifanya kilipaswa kufikirika kabla ya maamuzi ya kutenda, hivyo kukuletea shida katika kufanikisha mambo  pasipo kujua wapi walianza.

Wengine wanaishi maisha yao kwa kujiona, kujiona kwamba ndiye yeye,ukijiona kwamba u tajiri na wakati bado ukihitaji msaada na kuuacha uhalisia, kwamba kila kitu kipo sawa katika malengo na yale unayoyahitaji huku unasahau maisha yanakutegemea wewe, kwa lolote unalolitafuta na lenyewe linakutafuta, ni kama nguvu ya mvutano.

Hivyo ni lazima kuwa nalo jambo, acha kufanya lile lisilo na tamanio kwako na fanya kile unachoweza maana na chenyewe kitafanana nawe, ukitembea sana katika maisha utakutana na kauli ambazo nyingine zinasimamisha na kurudisha nyuma nafsi yako, ikiwa lakini yako utaitumia vizuri ukiangalia ni wapi utawekeza akili yako  na baadaye uyaache maamuzi yako yakikufata sambamba nawe.

Angalia katika njia ambayo unaweza kuyatengeza maisha yako yakawa vile utakavyo kama vile ukaamini kwamba ipo siku maisha yako yatakaa na kubadilika ukiamini unaweza kuyafanya maisha yako katika yale utakayo yakakurudia ama kukupata upya, kama hauna kitu nyanyuka na ukafuate kile unachokitaka.

Hutapoteza kile unachokitaka kipo na kinakusubiri wewe kama bado ulikuwa haujakipata,achana na mawazo ya kilichopotea maana unapoelekea ni mbele kupata maana amua sasa ili watu wengine waje wasome kupitia wewe.wengine wanasema hapana huku wakiwa hawajui kama wanakataa juu ya nini.

Nguvu iliyopo ndani yako ni kubwa,jiamini na safiri na nyota yako.

 

Sunday, September 25, 2016

FANYA LEO YAKO


Kuna Wakati mtu unakuwa na hofu ya kuishi na hali ya kutojiweza na kusema huwezi au kwa sababu ya hali na uchumi wa nchi ulivyo,matatizo binafsi na kukata tamaa,kuwa na tatizo lolote linalokufanya kuhofia kesho yako.

Inakupasa utafakari muda na uangalie ni vitu gani vinavyokushinda kuvifanya na kuvinakili pembeni nakuanza kufanya chaguzo katika lipi lile utakaloanza nalo maana utakuwa umeitumia leo yako tofauti na ilivyoifanye leo yako ikajenge kesho nzuri na ukitambua nini kazi ya maisha yako kama hauwezi kufanya mda flani basi japo kidogo.

Ufikirie ni nini maisha umeyaandalia katika muda wako husika hapa duniani,unaweza kujifariji kwa kile unachokiweza kufanya Leo kwa kutofanya na kusema utafanya kesho na usifanye tena,hii yaweza kukufanya usiwe na uhakika wa maisha yako na hata ifike kipindi usiamini kama ni wewe kwa kujiona bado wa jana,

Na ufikiri zaidi ni namna gani unaweza kuendesha maisha yako sio zaidi ya kuishi maisha yao,hii inapelekea na kutokana na  kuhairisha na kufa kwa ndoto kutokana na misongamano iliyopo katika mizunguko ya maisha,

Yakupasa kuzoea magumu kujua kwa nini haijafanyika na sio kulaumu kwa nini ulishindwa kufanya,fanya leo bado haujachelewa usiogope nafsi na macho ya watu wengine wanaokuzunguka,ukijua Leo wewe ni nani ukajua ni namna gani ulivyoachiwa jukumu La kufanya ndoto yako kuwa maisha kwa kuyatekeleza Yale unayoyategemea katika maisha yako.

Katika kufanya Leo yako Leo inahitaji ujiamini,ujisikilize na uisikie ile sauti inayokwambia kitu ndani ya moyo wako,yaache Yale yaliyolegea peke yake ukiwa umeyatilia maana ukiyaacha ndiyo utajua wewe ni nani maana kile kilicho na penda kitaashiria upendo ndani yake na kuonekana juu yako.

Usitumie muda wako kubishana na mtu yeyote hasa katika mambo yasiyo na msingi,kujua jambo la msingi ni kujua kile unachokihitaji,pengine usibishe usilolijua ,kuna vitu vingine unavichukua katika maisha yako na kuishi navyo lakini inapofika kipindi Fulani ni lazima kusema imetosha,

Ikitosha huwa inatosha,ni kama kushiba ilivyo tofauti na kuwa na njaa,maana ukishiba ukala tena basi kuna shida mbele yake,inaogopesha kuendelea na maisha huku fikra zako zikiwa zimezungukwa na hofu,wale watu wote wanaokuzunguka ni faraja tosha katika njia ya maisha yako kupitia kile unachokisema,unachokisikia na kukitenda juu yao na wao juu yako,

Ukiwa popote na nguvu ya kufanya lolote msingi ni kujiruhusu we we mwenyewe kufanya kitu Leo sio kwa kufikiria kilichokuwa kinafanyika zamani au wakina Fulani wanafanya nini.

Maisha ni kukua,kama hakuna kukua ni lazima kufikiri nini kinasimamisha pale kunapokuwa hapakui,Ndio maana yakuwa na kesho ambayo yaweza kuwa leo yako,Usichanganyikiwe kwa vile ulivyo na kile unachokifanya leo,weka ubongo wako kuwa  ardhi yenye hitaji la kupanda mbegu bora tena tofauti tofauti.

Amua kukua kwa njia na Mawazo sahihi na kufanya yale mazuri Leo tambua kila MTU ana mawazo mengi jaribu kile unachokiogopa na kataa sauti inayokukataza na amini kufanikiwa nacho,kufanya kwa kuweka mawazo mapya yanayoendana na maisha yako ,

Kupenda na kufanya linalotakiwa kwa  kuwa muwazi,mwaminifu na kuishi katika sababu na majibu yako,pale kwenye lawama ukaweka msahama, Nia thabiti katika kila njia upitayo bila kusahau kumshukuru  Mungu pale Uionapo Leo yako.




Saturday, September 24, 2016

BADILIKA.

KUNA KIPINDI UNAWEZA FIKA NA KUSHANGAA NAMNA YA JINSI MAISHA YAKO YALIVYO,YAKIWA YAMESIMAMA AU KWENDA VILE AMBAVYO HUJATEGEMEA WEWE, KUMBUKA KILE KINACHOKUSIMAMISHA NI KILE UNACHOKIFIRIA, PENGINE UNAJUA UNAPOHITAJI KUFIKA LAKINI HAUJUI SEHEMU ULIYOPO KUTOKEA PALE ULIPOANZA, KINACHOTAKIWA KUANGALIA NI NAMNA HALI YAKO ILIVYO, MAANA HALI YA MTU INAKUJA NA MTU MWENYEWE BAADA YA KUAMUA YALE ANAYOYAONA YAMEMJIA HASA KATIKA WAKATI ULIOPO, MWENGINE ATASEMA YEYE NI MTOTO WA PEKEE NA YULE ANAISHI MAHALA FULANI, AU MIMI BADO SIJAKUA..HIZI ZOTE ZIKIWA NI SAMAHANI ZA KUTAKA KUTOKUTENDA,BADILIKA NA FIKIRI MAISHA UPANDE WA MTU MWINGINE.

NIKIFANANISHA MAISHA KAMA MKONDO WA MTO, PENGINE UNAPOTILILISHA MAJI YAKE HAYACHAGUI NJIA YA KUPITA LAKINI YATAFIKA PALE YANAPOTAKIWA KUFIKA PALE NJIA ILIPOTENGENEZWA NA MAJI, HIVYO NJIA HALISI YA MABADILIKO ANATENGENEZA MTU MWENYEWE, UKIWA NA LENGO LA KUULETA UKWELI WA MAISHA YAKO.HIVI SASA KAMA ULIKUWA BADO UNAHITAJI LA KUFIKIRI NI NAMNA GANI UTAWEZA KUYABADILISHA MAISHA YAKO, MATATIZO KUWA STAREHE, NA KUJIPELEKA MWENYEWE KATIKA DARAJA LINGINE LA JUU ZAIDI ULIYOPO.JARIBU KUFANYA KILE UNACHOHISI NI MAENDELEO, KINACHOWEZA KUKUONGEZEA THAMANI NA NGUVU KATIKA MAISHA YAKO,FIKIRI YALE YALIYOFANYIKA MIAKA YA 70 NA SASA NI SAWA SAWA PENGINE WATU NI TOFAUTI,AU NI TOFAUTI NA WATU NI SAWA SAWA,USIKUBALI KUWA MTU YULE YULE,YULE WA SIKU ILE,FANYA MAZURI KWA WATU AMUA,BADILISHA NAMNA NA TEMBEA UKIJUA ULIPOTOKA,ULIPO NA UNAPOKWENDA

JAZA UBONGO WAKO NA YALE MAZURI, YALE YALIYO NA WELEDI WA KUWEZA KUUFANYA UBONGO UKAWEZA  KUKUVUSHA KATIKA YALE MAGUMU,PANGA NA AMUA KUFANYA KATIKA KUELEKEA MAENDELEO INGAWA DUNIANI KUNA ATHARI NYINGI AMBAZO KIMSINGI ZINATUKABILI NA HIZO HUWA NI CHANGAMOTO KATIKA MAISHA,FUNGUA UBONGO WAKO NA KUYAFANYA  MAISHA YAKO YAWE YENYE NGUVU NA MAANA,FUNGUO HIYO NI MAAMUZI YA KUJIAMBIA KILA SIKU IENDAYO KWA MUNGU KUWA INAWEZEKANA,INAWEZEKANA KUBADILI KILE UNACHOKIFIKIRIA KWANI KUJUA KAMA INAWEZEKANA NI MABADILIKO TOSHA.

@Benson Makaya

Friday, September 23, 2016

MAAMUZI

FIKIRI KILE AMBACHO UNAKITAKA KUKIFANYA, PENGINE UKIWA UMEBAKI NYUMA KATIKA KULIFANYA JAMBO HILO KWA SABABU FULANI HUSIKA, SIYO KWAMBA BINAFSI HAUKUWA NA HITAJI LA KUFANYA JAMBO HILO LAKINI CHANGAMOTO ZA MAISHA ZIKAKUCHANGANYA NA KULETA MAJIBU TOFAUTI PENGINE UKAWAZA NA KUONA KAMA HAUKUTAKIWA KUFANYA WEWE KWA VILE LILE JAMBO LIMEKUWA NI GUMU, UKAOGOPA KUFANYA JAMBO KWA KUWA UTAFELI SANA, PENGINE UMEWAFERISHA WENGI SANA HAPO NYAKATI ZA NYUMA.

MTU HANA MAAMUZI YA KUFANYA MAAMUZI, KUAMUA KUFANYA MAAMUZI NI KUAMUA, KUNA YALE MAAMUZI MADOGO AMBAYO WENGI WETU TUNAYAACHA KWA KUWA HATUYAJARI HAYO MADOGO,LAKINI MADOGO HAYO NDIYO HUWA MAKUBWA BAADAYE,INGAWA PIA KUAMUA KUTENDA NI CHANGAMOTO KUBWA SANA, KAMA MAMBO YANATOKEA KATIKA MAISHA YETU KATIKA KUFANYA YALE MAMBO AMBAYO MTU UMEKUSUDIA KUFANYA LAKINI KATIKA NAMNA MOJA AMA NYINGINE UMEKUWA NYUMA NA HAUJAFANIKIWA KUFANYA, NA UKITAMBUA NI LAZIMA KUFANYA LAKINI HUJAFANYA, KILA MTU ANAJUA SIO RAHISI, SIO RAHISI KUFANYA JAMBO GUMU.

KATIKA VITU VINAVYOTUFANYA BINADAMU KUWA NA HOFU YA KUTOKUFAULU NA KUFELI PENGINE HUWA NI KWA KUPOTELEWA NA MTU AU KITU KINGINE,KUDHARAULIWA,IKIWA HIVYO KWA MUDA MWINGINE INAKUPASA KUJUA KWA NINI UNAFELI,NA KAMA NI HOFU UKAISEMA MAANA HOFU HUWA HAITOKI KATIKA MAZINGINRA YA BINADAMU,HUTUZUNGUKA.HII INAWEZA KUKUPELEKEA KULAUMU NA KUJINYIMA UWEZO WAKO WA KUWEZA KUFURAHI.SIO KWA SABABU MMOJA NI MZURI NA MWENGINE NI TOFAUTI HAPA UKUMBUKE HAKUNA LILILOKAMILIKA DUNIANI LAKINI KUPITIA USEMI HUU SI YA KUMAANISHA SIO KWA SABABU YA HIYO NDIYO NAWE UWE,FIKIRI MANGAPI HUJAFANYA,MANGAPI HAUJAYAMALIZA..USIYAOGOPE NA YAFANYE SASA NA BAADAYE UTAONA UYAFANYAYO YATAKAVOAMISHA MAISHA YAKO.

WATU WENGI HAWAPENDI KUFANYA MAAMUZI MAGUMU KWA SABABU WANATAKA WAFANYE MAAMUZI SAHIHI KWAO.KUFANYA MAAMUZI KUNAHITAJI NGUVU,SASA HIVI AMUA NI KIPI UWEZE KUWEKA NIA  YAKO,UKIWEZA KUWEKA NIA KATIKA LILE ZURI NDIYO PALE UJUZI WAKO UTAKAPOONEKANA.


BADILIKA NA FANYA MAAMUZI SASA.

@Benson Makaya:

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...