Sunday, September 25, 2016

FANYA LEO YAKO


Kuna Wakati mtu unakuwa na hofu ya kuishi na hali ya kutojiweza na kusema huwezi au kwa sababu ya hali na uchumi wa nchi ulivyo,matatizo binafsi na kukata tamaa,kuwa na tatizo lolote linalokufanya kuhofia kesho yako.

Inakupasa utafakari muda na uangalie ni vitu gani vinavyokushinda kuvifanya na kuvinakili pembeni nakuanza kufanya chaguzo katika lipi lile utakaloanza nalo maana utakuwa umeitumia leo yako tofauti na ilivyoifanye leo yako ikajenge kesho nzuri na ukitambua nini kazi ya maisha yako kama hauwezi kufanya mda flani basi japo kidogo.

Ufikirie ni nini maisha umeyaandalia katika muda wako husika hapa duniani,unaweza kujifariji kwa kile unachokiweza kufanya Leo kwa kutofanya na kusema utafanya kesho na usifanye tena,hii yaweza kukufanya usiwe na uhakika wa maisha yako na hata ifike kipindi usiamini kama ni wewe kwa kujiona bado wa jana,

Na ufikiri zaidi ni namna gani unaweza kuendesha maisha yako sio zaidi ya kuishi maisha yao,hii inapelekea na kutokana na  kuhairisha na kufa kwa ndoto kutokana na misongamano iliyopo katika mizunguko ya maisha,

Yakupasa kuzoea magumu kujua kwa nini haijafanyika na sio kulaumu kwa nini ulishindwa kufanya,fanya leo bado haujachelewa usiogope nafsi na macho ya watu wengine wanaokuzunguka,ukijua Leo wewe ni nani ukajua ni namna gani ulivyoachiwa jukumu La kufanya ndoto yako kuwa maisha kwa kuyatekeleza Yale unayoyategemea katika maisha yako.

Katika kufanya Leo yako Leo inahitaji ujiamini,ujisikilize na uisikie ile sauti inayokwambia kitu ndani ya moyo wako,yaache Yale yaliyolegea peke yake ukiwa umeyatilia maana ukiyaacha ndiyo utajua wewe ni nani maana kile kilicho na penda kitaashiria upendo ndani yake na kuonekana juu yako.

Usitumie muda wako kubishana na mtu yeyote hasa katika mambo yasiyo na msingi,kujua jambo la msingi ni kujua kile unachokihitaji,pengine usibishe usilolijua ,kuna vitu vingine unavichukua katika maisha yako na kuishi navyo lakini inapofika kipindi Fulani ni lazima kusema imetosha,

Ikitosha huwa inatosha,ni kama kushiba ilivyo tofauti na kuwa na njaa,maana ukishiba ukala tena basi kuna shida mbele yake,inaogopesha kuendelea na maisha huku fikra zako zikiwa zimezungukwa na hofu,wale watu wote wanaokuzunguka ni faraja tosha katika njia ya maisha yako kupitia kile unachokisema,unachokisikia na kukitenda juu yao na wao juu yako,

Ukiwa popote na nguvu ya kufanya lolote msingi ni kujiruhusu we we mwenyewe kufanya kitu Leo sio kwa kufikiria kilichokuwa kinafanyika zamani au wakina Fulani wanafanya nini.

Maisha ni kukua,kama hakuna kukua ni lazima kufikiri nini kinasimamisha pale kunapokuwa hapakui,Ndio maana yakuwa na kesho ambayo yaweza kuwa leo yako,Usichanganyikiwe kwa vile ulivyo na kile unachokifanya leo,weka ubongo wako kuwa  ardhi yenye hitaji la kupanda mbegu bora tena tofauti tofauti.

Amua kukua kwa njia na Mawazo sahihi na kufanya yale mazuri Leo tambua kila MTU ana mawazo mengi jaribu kile unachokiogopa na kataa sauti inayokukataza na amini kufanikiwa nacho,kufanya kwa kuweka mawazo mapya yanayoendana na maisha yako ,

Kupenda na kufanya linalotakiwa kwa  kuwa muwazi,mwaminifu na kuishi katika sababu na majibu yako,pale kwenye lawama ukaweka msahama, Nia thabiti katika kila njia upitayo bila kusahau kumshukuru  Mungu pale Uionapo Leo yako.




No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...