Hasa pale ukafika wakati maana ni wazi hata ukiwa mfalme inapasa kuunyofoa ufalme wako,ilifika kipindi kuonekana kufungwa njia katika baadhi ya sehemu,ikiashiria hatari ama kirahisi zaidi ikawa si ruksa kupita,lakini ukiwa mfalme unaruhusiwa kwa kuwa wewe ni mkubwa,zama za kizamani sana ambazo zinafanya watu kuendelea kunyonywa bila ya kujua,eti leo ukapange foleni kwa kuwa umekatika mguu na mwengine akaje ya kuwa jana alikuwa akichezea mtoto kwenye vumbi basi mafua yamemshika sana anaomba kupita,kwa maana ana ahadi na daktari.
Kali chache kuliko chungu,maana chungu hazina utamu kama ukali wa uchungu,ikiwa inatakiwa kutizamia mbele siyo kwa kuwa ndiyo unapoelekea,kwani hapo yapasa kutazamia namna ya mwelekeo.ufalme umetawala kwa kila asiye mfalme maana kwa kwenda na nyakati imeonekana ni kheri kuhifadhi kuliko kuweka kwani zikijaa mfalme anaweza kuziihitaji kwa kauli inayosemeka kama amri.
Pengine leo ikakupase uone ufalme wako,leo ukajifanye ni mfalme wa mambo yako kwani ikiwa tangia uwe mtoa huduma hujafikiri kuunyofoa ufalme,kuondoa lile lililo na uhakika wa kukaa milele kwa vile litajirudia tena,kwa nafasi za ufalme zilizotengwa imeonekana wazi unatembea katika reli isiyokuwa kama tazara..maana unawezajishirikisha kwa kujiona Mfalme bila kujua namna gani ya kuweza kuunyofoa,si mbaya kwa usiye jua kujifanya unajua,maana ndiyo nguvu ya mfalme Juha.