Kichwa kinajaa mengi kutokana na namna ya mtu
unavyokuwa,ukiwa umelala kubali kuota ndoto maana ndiyo sehemu yake,unaweza
kuota mchana kuwa usiku,hapa ni pale unapoiamini ndoto ya uwongo kuwa ya
kweli,yaani ni sawa na kulazimisha kuvaa nguo ya mtoto ya jinsia tofauti,sijui
ikichanika labda italeta maana,maana wengine huwa kazini wakifanya yao,pengine
ukiwa kazini ukifanya yako,yakajaa pengine ya kuwa hakuna sehemu ya hifadhi
basi yakabaki katika hifadhi ya kuingia na kutoka.
Hapa mawazo yanaweza kuongezeka zaidi,maana unaweza kuona
kile ambacho hujawai kukiona na kukuta kwamba ni kweli ilipasa kukiona,maana
ukiwa hujakiona basi utakiona,hapo ni sawa na mtoto kabla ya ukubwa,ni sawa na
mzazi kabla ya uzazi,maana vyote vinapotokea hutokea si katika namna ya
kuumizana,bali katika namna ambayo kichwa kinaweza kuyafikiria,kichwa hufikiri
kutokana na mtu mwenyewe na wala siyo kitu,maana inaweza kutokea hatari ya
kukimbia na kila mtu akakimbia kivyake,hapo kila mtu akiwa ameyajaza yake
katika kichwa chake.maana ya mbio kujulikana ni tofauti.mtu hufahamu ukweli wa
kitu kwa vile anavyofahamu yeye.
Hakuna maigizo yanayoweza kuja bila kutoka
kichwani,haimaanishi kuigiza kwa vile tunavyofikiria kwa kuanza kutafuta vile
vya kweli,ukiwa na imani ya kuona utaona maana kuna walioona lakini hawakuweza
kuona,hivyo nikiwa na maana ya nafsi na kichwa cha mtu mwenyewe
alivyokijaza,ukijaza mchanga kichwani lazima utakuta umesambazwa na
machozi,maana unapofika wakati wa mlima na hata pale wakati wa mteremko,kukiwa
na mengi sana mengine hayapaswi kufikirika ikiwa siyo chaguzi lako.
No comments:
Post a Comment