Wednesday, October 17, 2012

MBADALA....

Hapa nikiwa nataka mabadiliko,yaliyo katika mazungumzo ama yakabadilika yenyewe kutokana na mfumo wa kubadilisha badilisha unavyoleta mabadiliko,pengine nikiwa sitaki kutoka kwa kuwa kuna mbadala basi ikaje zamu yangu nikaamua kutoka kwa kuwa ilitakiwa kubadilika,kubadilishana maana kukiwa kuna kitu kilishikiliwa,unaweza  unayoyafanya yakawa siyo yale yanayofanyika,hapo mambo yatabadilika kwa matokea halisia.
 
 
Wengi wao wengine hao hufikiri kile cha mtu ndiyo chao,hapo wakifanya mbadala,maana kuna kuwa na mbadala wa kufikiri katika kile kizuri ama kibaya ikiwa vyote ni vitu lakini kukawa na mbadala wa mawazo katika kujua kile ni kizuri ama ni kibaya,pengine ikawa ni kizuri kile kilichosememwa ni kibaya,hapo  ni baada ya kizuri kufanya mbadala na kibaya,pengine endapo  mazingira yamesema.na hapo kunakuwa na mbadala zaidi kwa pale utakapotaka kusema mwenyewe ikiwa tayari mazingira yalishasema..
 
 
Kesho isingeweza kuja bila kubadilishana na siku njema ya leo,hapa ukisema bora kesho maana ya kutokuielewa leo,ama ukaielewa kwa kubadilishana na fikra za kutokuelewa,hapa ukiwa umefanya mbadala wa fikra na zaidi ikatokea katika matendo,kwani mwanzo ilisemwa kwa kuwapo na jambo Fulani,na ukiona mwisho umekuja jua lazima kuna mabadiliko,hayo yakiwa kama siyo kimatendo basi ni namna ya muda ulivyotumika.

No comments:

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...