Wakati na muda unavyokwenda…kwa kuongea mazuri ama vile ukaja muda ikatulazimu kufanya,ikiwa
mwengine akilalama kwa kuzungumza sana akiwa na maana ya kuchoka ya kuwa
amezidisha,ukiwa hauhitaji kuongea sana zaidi ya jambo kutendeka,hapa wachache
wakikuangalia kama umeweza ama ulikuwa umezungumza tu,hapa wachache
watakushangilia ya kuwa umetenda kweli,licha ya kuweza kutokana na baadhi ya
nafsi kushindwa kutimiza malengo waliyonayo,na hiyo siyo kwamba wamekuwa
wakisema sema bila kufanya,pengine yapasa kufahamu cha kufanya kabla ya
kuzungumza.
Mara nyingine itakuja kipindi hata yale yasiyo kuwa na maana
kwa mtu mmoja kutendeka kwa kuwa mtu
aliyezungumzia ni wa maana,bila kufikiri unaweza kulamba kalata dume,pengine
hata ukiwa na mapenzi na hilo dume kwa kuwa na uzalishaji lakini kuna nyingine
hufanyika kwa kuwa wachache walishafikiria mwanzo,tena tofauti si kama ilivyozoeleka,hakatazwi mtu kusema bata ni
kuku,maana hapo inahitajika sababu,ikiwa kuna wale watakao pata kuwa bata ni
kuku na wapo watakao kosa ya kuwa kweli bata si kuku.tunahitaji mazungumzo
mazuri.
Hii imekuwa kama chaguzi maana kuna wengine hutumia
kuzungumza wakiwa hawana ya kutenda,kama vifaa hakuna yapasa kuomba kwa jirani
akiwa hana kazi navyo,maana baadaye anaweza kusema kwanini hukusema mwanzo,bila
kudhani kama mwisho wake ndiyo umefika au ni mwanzo wenyewe maana kuna
kuchelewa,,leo unahitaji kusema maana pengine hata ya moyoni yatatoka ikiwa
yana milango yake,unapozungumza jaribu kuuweka kuwa ni moyo umezungumza .maana
japo tutasubiri kwa kauli ya upendo utakaposema kusubiri.
No comments:
Post a Comment