Monday, October 8, 2012

PESA..


Nikisema iilkuwa wakati wa matumizi nitadanganya umma,ila kama sikuweza kusikia basi kushuhudia baadhi ya matukio ya kipindi icho,vijana wa kisasa wanasema wanakumbuka enzi zao,enzi ni nyuma na ujenzi,maana inawezekana enzi zikawa ni nzuri kuliko ujenzi,unaweza kujenga kile usichikitegemea na bila kujua utachanganyikiwa kwa kuporomoka hadi kujikuta huna maana kabisa..kile kinachopoteza hata thamani ya kukopeshwa hicho kitabaki na maana pekee,pengine ikiwa wanaotumia hawana maana pia,bora kuwa hauna maana kuliko kufanyishwa hauna maana.

Wengine watasema naleta vita kwani wao wameshazoea kama miaka ile ya 75,unajua ili kubadilisha namna ya kukaa ni kumweka adui pembeni,dawa ya adui hakuna asiyeijua kama siyo aibu za kuoneana rangi,ikiwa moja imependeza na nyingine imeiva,zote nzuri tuangalie wasije badilisha mpaka zikawa sita maana kila kijiji itabidi kitumie pesa zake,tena  karatasi za kuingilia na kutoka’ zikae sawa maana mda si mrefu adui anaiporomosha thamani.

Nimebaki na maswali mawili matatu yanayonishusha thamani,pengine kujumlisha ni kutoa,maana ikiwa kukuwa kwa mgomba ni kukomaa lazima tuangalie na virutubisho,unaweza kukua mwili tu..leo ukajibadilisha rangi hii,kesho ukaona upendeze na nani na fulani…yote yako hayo,kama unazo zaidi ya moja zenye thamani moja mpe hata wa jirani ya mbali ya nchi nyingine pengine zinaweza kupanda thamani zikiwa huko maana nabii hasifiki kwao.

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...