Nashangaa sana kuona watu wakiangaika na katiba ikifika muda
wa kenda miaka sasa,nashindwa kuelewa nilichosomea ni nini maana ni wazi siwezi
kuandika katiba,hapa lazima nikuulize kijana mwenzangu ikiwa ni utani kwa mzee
akimwambia kijana mwenzangu..sikuweza kufikiri wala kujua endapo piki piki hizi
za wachina zinavyotenegenezwa kwa wingi na kuingia kama karanga,ushuru bure
kama unapeleka kule,leo ije waseme hakuna spea,hizo zikiaribika ndiyo mwisho wa
safari yake ya maisha,wakisahau jamani hizi pikipiki ndiyo zinazotuendesha,wakisahau
yaliyo katika katiba ndiyo yanayotuendesha,tena siyo kibinafsi.
.
Tumezoea kuendesha bila kujua kama tunaendeshwa,kama swala
ni kukubariana basi liwekeni kwa wananchi watamtafuta aliyeitunga ya
kwanza,maana nashangaa kila siku kubishana,yaani kama ulikuwa unaishia
vizuri,sasa unang’ang’ania kuishi vibaya,wewe kijana angalia usije kufa umri si
wako,wazee mnayafahamu haya ila hampaswi kuitwa wapumbavu.usitegemee kufa kwani
ni bahati mbaya,kama unauwezo amka kesho nenda kajikwae barabarani,na wala
siyo lazima iwe kwa wote,
Nina imani ya kuwa na wengi walio soma na wasijue wamesoma
nini,hili ni kosa la kutokuambiwa kama ubongo hautanuliwi na ulimi,ni namna ya
kuuweka makini,ili kesho-kesho kutwa isije ikaja usiamini.unawezashindwa
kuelewa ni kwanini yale maneno yamekutazamia wewe,maana hata kama ni mimi
lakini ni namna unavyoichukulia wewe,huu ni uswahili na haina kustaajabu yaliyo na vituko uswahilini.
No comments:
Post a Comment