Saturday, August 25, 2012

TENDA WEMA NENDA ZAKO..


Hulazimishwi kulia na wakati wewe unataka kufurahi na kucheka,swala la msingi ni kujua unapokatazwa kulia,hapa nikiwa sina maana ya kuhudhunika kwa lile linalokwaza,hakuna baya alitendalo mwanadamu zaidi ya Mungu mwenyewe kujua,maana imekuwa hata nafsi yenyewe ikajitendea mabaya ikiwa wema umezidi sana,maana binadamu umekua unayashika mabaya kuliko yale yaliyo mema ikiwa mabaya hayo yanahesabika ujiulizie mazuri ili ukayatende na uende zako,hapa mtu ukiwa na lengo la kutaka kujua,na sio kushabikia kwani unaweza kushabikia timu alafu ikawa inafungwa kila siku ni sawa na kumsaidia mtu kila siku alafu mwishoni anakufukuza kama mbwa,yakupasa kuacha kushabikia usivyovijua.

Adhabu zote yakupasa kuzitumikia kwani maumivu hujenga,lakini si katika namna ya kutaka kuishi na adhabu hiyo hata kama mema yanahitajika,mwanadamu kila siku anakuwa kwa kusikia na kuona pia unaambiwa maneno mengine siyo ya kuwaambia watoto wako wakiwa hawatakiwi kujua menigne yale,ingawaje ni vyema kumjuza mtoto ili naye akikuwa akatende yale tu yaliyo mema kwake na yakuwa wanadamu hatuna dogo yakupasa kutazama pande ya kule na huku alimradi ikufae.

Shukuru mungu yakuwa unapumua mengine ni ya dunia,songa mbele usikate tamaa kwa kwenda na bila kutenda,kwenda zako isichukulike hasira kwani kesho na kesho kutwa mjinga atafahamu kuandika na kusema shukrani,Mbinguni unaenda kwa ajili ya mazuri na mabaya yako,kama mtu unaamini kule atapata adhabu kwa mabaya yako basi ujue hayo ni ya Mungu asiyoyaruhusu wakati huu uliyasikia lakini hukuyafanyia kazi ama uliyafanyia kazi lakini si sahihi na vile ilivyotakiwa,ya binadamu yanaisha hapa hapa duniani,unapaswa kuwa mwema ili kufanikiwa vyema katika maisha yako na kuleta amani ya moyo na fikra iliyo na  mafanikio makubwa.

MAAJABU...



Kwa Mungu kila goti litapigwa,kila anayetenda atende akijua kwa maana ya kutokupiga magoti tofauti,unaweza kuwa mitamboni na kushindwa kufanya yale yanayotakiwa,pengine ukiwaza mengine ni magumu bila ya kuyapigia goti maana yamekuja yenyewe na kuonekana maajabu,kumbe maajabu ni yale yasiyo na muonekano mzuri pengine ukayashindwa au kufanya wachache kwao ndiyo ikaeleweke kama yalitendeka,imekuwa maajabu ni kitu cha kawaida na hiyo sio kwa upande wangu tu,pengine ikawa haifahamiki,haina haja ya kuumia na wakati inaonekana jambo fulani ni la ajabu,ili labda wengine wasithubutu,maana ukaambiwe ujaribu kwanza.

Katika yale yaliyo marahisi hata yale maajabu huwamo,maana mengine yanahitaji mazoea kwanza,pengine bila kudhani kudharirishwa zaidi ya kuwa shujaa,pengine ukajidharirisha mwenyewe,kwa kuangalia yaliyo ya ajabu unaweza kuona vyema,na hiyo vyema kuja na kuwa uwongo,hapo ukiwa umedanganywa na macho,maana yenyewe yanaona kila kitu,pengine yangekuwa yanachagua basi maajabu yasingeonekana ya nini sasa?

Moyo hufurahi kwa lile linalotendeka,hata likiwa chafu kwa mwengine lakini safi kwako,hii ikiwa unaye ishi ni wewe,pengine hujui kuwa na wengine wanaishi,tena siyo kama wewe wao ni kiajabu ajabu,maana ungelielewa hilo mwanzo.machache yaliyotangulia ndiyo katika yale machache ya maajabu,maana kuna maajabu mengi sana duniani hapa,ikiwa na yenyewe yaliumbwa,hayakuumbwa nasi bali yanakuwa kutokana na sisi.pengine ungalikuwa mtoto bado ungetueleza maajabu uliyotumia kuyaangalia mpaka ulipofikia umri wako,

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...