Kwa Mungu kila goti litapigwa,kila anayetenda atende akijua
kwa maana ya kutokupiga magoti tofauti,unaweza kuwa mitamboni na kushindwa
kufanya yale yanayotakiwa,pengine ukiwaza mengine ni magumu bila ya kuyapigia
goti maana yamekuja yenyewe na kuonekana maajabu,kumbe maajabu ni yale yasiyo
na muonekano mzuri pengine ukayashindwa au kufanya wachache kwao ndiyo
ikaeleweke kama yalitendeka,imekuwa maajabu ni kitu cha kawaida na hiyo sio kwa
upande wangu tu,pengine ikawa haifahamiki,haina haja ya kuumia na wakati
inaonekana jambo fulani ni la ajabu,ili labda wengine wasithubutu,maana
ukaambiwe ujaribu kwanza.
Katika yale yaliyo marahisi hata yale maajabu huwamo,maana
mengine yanahitaji mazoea kwanza,pengine bila kudhani kudharirishwa zaidi ya
kuwa shujaa,pengine ukajidharirisha mwenyewe,kwa kuangalia yaliyo ya ajabu
unaweza kuona vyema,na hiyo vyema kuja na kuwa uwongo,hapo ukiwa umedanganywa
na macho,maana yenyewe yanaona kila kitu,pengine yangekuwa yanachagua basi
maajabu yasingeonekana ya nini sasa?
Moyo hufurahi kwa lile linalotendeka,hata likiwa chafu kwa
mwengine lakini safi kwako,hii ikiwa unaye ishi ni wewe,pengine hujui kuwa na
wengine wanaishi,tena siyo kama wewe wao ni kiajabu ajabu,maana ungelielewa
hilo mwanzo.machache yaliyotangulia ndiyo katika yale machache ya maajabu,maana
kuna maajabu mengi sana duniani hapa,ikiwa na yenyewe yaliumbwa,hayakuumbwa
nasi bali yanakuwa kutokana na sisi.pengine ungalikuwa mtoto bado ungetueleza
maajabu uliyotumia kuyaangalia mpaka ulipofikia umri wako,
No comments:
Post a Comment