Thursday, August 23, 2012

SUBIRA HUVUTA KHERI


Kheri huletwa na mwenyezi mungu,mwanadamu ana kheri ya kuwa na pumzi ambayo humfanya akaweza vile awezavyo kwa Kheri yake Muumba,unaweza kusubiri  mpaka tumbo likauma mambo mengine hayana subira,mwanzo ukiwa mgumu haimaanishi kwamba mwishoni ni neema ikawe kwa subira na kuupoteza muda,pengine usipojua subira nyingine bado hazijafanyika,unaweza kupoteza ukisubiri tena sio sana ama ikawa kheri kwa kuwa mmoja alisubiria,leo upoteze vurugu kwa kuwa na subira,usiseme tu kama iwavyo kwa dalili ya mvua,labda ukiwa unahitaji mazao mengi kwa pale ulipoandaa shamba lako

Iwapo kusema kabla ya tendo ni dhambi na uongo usingekuwepo,dhambi nyingi tu.
usisubiri ufike muda ili uanze kudanganya vyema,haina budi kusubiria maisha na kusema Mungu atakupa,hii ikiwa wewe ndiye unaye yaendesha maisha yako kwa kuwa Kheri ulishapewa,kuendesha taratibu ni sawa na kumsubiri abiria wakati wengine wanaharaka,hivyo bora utumie mwendo kasi unaokufaa, kama umechelewa utaenda na usafiri mwengine,uyape majina na rangi ili uweze kujua,kuwepo na subira zako za kutaka kuona na kujua,vingine ukiwa na subira za kutaka kuyaona maisha magumu yako wapi kwa udanganyifu wa kulipia subira pamoja na manung'uniko.

Huu ni mwanzo,sijui unaishi unategemea kufika mpaka mwisho upi,ama unaishi kusema kwamba leo au kesho kitalika nini,pamoja na ada ya watoto,si shule tu maana hata pumzi inalipiwa siku zote.kwa walio wengi wanajua kile wanachokitafuta maana kila aliye na chake akitumie,ikiwa ni macho kuona ama akili kufikiri,mengi yanatokana ikiwa umeamua mwenyewe kufanya,yaani ni unataka nini  maishani mwako,pengine ndiyo mlengo wa maumbo na thamani tofauti tofauti,na hivyo hauzaliwi navyo ukavikuta zaidi ya kusubiri na kuona yanayojiri,pengine haina haja ya kusubiri ikiwa yanayojiri yanaletwa na wewe wenyewe.

No comments:

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...