Kufikiri ni kuwa na hitaji la kurekebisha
jambo,kunatokana na mawazo,kwa hiyo fikra zinaweza kuwa ni mawazo,kufikiri ni
kitendo,kurekebisha ni kufanya,fikra hujaza matendo hayo,zikiwa kama fikra
halisi huwa haina ulazima ya kuwa iwe vile ama hivi,itakavyo kuwapo ndiyo
hivyo,ya kuwa kila mtu ana fikra zake,akiwa na malengo mwanadamu hupanua fikra
ili kuyafikia,hiyo yote ikiwa tunaamini kwa yale tunayotaka yatokee katika
mandhari yetu ikiwa ni baada ya matendo yetu au yenyewe tunayoyafikiria yatokee
ndiyo tutende,tunapotaka kuyafikia yale yaliyo mema,fikra zetu ndiyo huonyesha
usahihi wetu,fikra ndiyo zinatutambulisha kwani inasemeka kwa kile tunachokifikiria
ndiyo hasa tutakacho kitenda ikiwa tu kimeonekana. Mara nyingine kisionekane
kwa Yule anayetenda na hiyo inatokana na kuwa haijulikani,Yule anayetenda anaweza kuwa na ufahamu mdogo ingawaje yeye
mwenyewe akiona anaweza,kwa muonekano ni
wengi tunaweza,ndiyo maana ikawa fikra
zetu zikatutuma mahala na muda tofauti.
Mara nyingi tumekuwa tukikaa na fikra zetu,tukiziamini
ndiyo zenyewe,ingawaje vile vya mtu anapewa yeye mwenyewe,ikiwa tunavitenda au
tuonyeshe maana ya kile tunachokitenda,mabovu yapo mengi sana,ikiwa na mazima
yapo,mabovu ni haya hasa tunayoyafanya kwa kila fikra za kila mmoja wetu ikiwa
kwa Yule anayefanya pia naye anasema yake ni mazuri sasa sijui tunayafuata
yapi,hata kama sio ya kuyafuata tufikiri tumeyafuata mangapi mpaka hapa tulipo,maana
tusingeweza fika katika wakati huu bila kujua ni wapi tumetoka,hata tunapoenda
tutayafanyaje hayo?basi tuyaangalie yale machache waliyofanya wengine yakaitwa
ni mazuri,maana hata tukiwafuata watu wazuri tutakuwa kama wao zaidi kibaya
kinakuja pale tutakapo fikiri zaidi,na hapo tutakuta kuna upande mmoja
umetokezea katika upande mmoja ule mwingine wa kwanza,yaani nafsi moja imekuwa
kupitia nyingine,na mara nyingine nafsi itakayo iga isifanye vizuri vile
ilivyofanya ya kwanza,hapa tutachafua hata wale tuliowaita
watakatifu,tutawakuza zaidi wale tunaohitaji kuwaita watakatifu ikiwa hata kwa
Yule aliye fuata muelekeo alifuata njia nyingine,ni haki kutumia njia yako pale
ufanyapo ili mradi jibu liwe sawa,hii ni katika maisha na sio darasani..maisha
ni kama darasa.labda tuone utofauti wa walimu,wanafunzi,majengo na mazingira
yote ya shule hii iitwayo maisha,maana kwa upande mwingine mazingira
yanachanganya.
Kama shule ilishindikana ni vigumu kwa mtu kumweleza
fikra ni nini,sio kwamba haiwezekani,ila inaweza kushindikana kuelewa ikiwa
fikra ni tofauti,sio kama 1+1=2 au hesabu ya kinamna yeyote ili lije jibu
ambalo kwa aliyefundishwa anajua,au atakuwa amesahau,ikafike kipindi tukaelewe
ni namna gani tunaweza kuziendesha fikra zetu,binadamu tunaishi tofauti na hii inatokana
na fikra,ikuzwapo fikra ya mtu mmoja ni tofauti na mwingine,labda tuambiane
kuhusu ukuaji wa fikra zetu,isije tukashindwa na hili darasa la maisha kwa
kutaka tuelewe namna ambayo fikra ya mmoja ikataka tuelewe hivyo,lengo ni
kuelewa,na hili kuelewa inakupasa uelewe,vile inavyokuwa tofauti ndiyo njia ya
kupanua uelewa,kwani utofauti unakuja pale mtu anapoelewa sahihi,na ikiwa mtu
ameiona tofauti basi hataweza kuitenda tena tofauti labda iwe fikra zake
zimemtuma,na sio kwa Yule anayetaka kuelewa,kwa wengine imekuwa ni vigumu,wao
wakitaka kuelewa namna ile wanavyoelewa wao,tunapofika hapo tunakuwa
hatueleweshani wala hakuna maelewano, kwani kila mtu anaelewa lake zaidi ni
tujue lipi ni la msingi tutalazimisha kuongea ili ieleweke kuna maelewano lakini watakaoelewa ni wale hasa
wanaolazimisha,maana walikua na nia hiyo ya kueleweka kinamna yeyote
walivyolazimisha.
By: Benson
G. Makaya,
Tel: +255 71 33 66 57.
Email;bensonsmakaya@gmail.com
No comments:
Post a Comment