Sunday, June 3, 2012

MY DEAR YUNIA

ni salamu bora kwa ajili yako,pengine uangalie chini na kukaa kitako,ni  gharama kubwa sana 
kwa zawadi yako,hakika unamtukuza mungu wako pengine ni zile aina na namna zako subiri leo uone kesho yako si kutishana bali ni habari zako,mungu wasaidie wengine hata watembeako,muda mwingi  pale jua lizamapo,Kuitana wifi na rafiki zako madada zangu ndiyo wale rafiki zako ntaongea mengi temeke sijafika labda gongo la mboto,ningeona tofauti kwa yale mambo yako,mapenzi bora hujulikana yatokeapo,mapenzi bora ni kwa mtoto wako,nafsi zikaungane na kuwa zako maana ya muunganiko wangu kutoka kwako,maisha ni mafupi tule kiapo,maisha ni matamu japo tuyaonjapo.ufikiri mbele na sio utokako,tufikiri mazuri mpaka tufanikiwapo

Imani yangu ni katika ndoto zako imani yangu ni katika ukifanyacho,maana umekuwa kidonda ,hata ukauma kwa utamu,Mawazo yako yameniinua,nimekuwa mpana wa kufikiri kwa kuona wale wanaotaka kukununua,pengine isiwe siri kuona ama tukaona kwa vile tukasikia,hapa utasikia machache sana kwa kubania  yaliyomuhimu maana imekuja wakati chako kikawa kizuri zaidi,yaani umepitiliza katika unyoofu niliouzoea katika mambo niliyoyategemea,umekuwa kibiriti kwangu my dear,umeniwasha na mwisho nikamalizika umenipuliza kabisa,umeniwasha asante kwa kuitikia,umenilaza na asante kwa kuitikia.

Maisha yamekuwa bora kwangu nahitaji kukutumikia,umekuwa kinara wangu kwa mataa kunimulikia umeniwasha kupindukia,nalijaribu kuangalia pembeni sikusikia,kabla sijasikia ya nani ntayafikiria?umemaliza mawazo kwa machache kuchangia ,unyooshe kijiko ya kuwa sukari yenyewe ni ndogo ya kurumangia ,mtamu usipungue kamwe nawe enedelea kunibembeleza,sipati raha lakini moyoni najisikia,nafsi yangu umeiweka angani mwezi na jua havijulikani


Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...