Thursday, November 15, 2012

JIONGEZE



Endapo hata ukiwa na chaguzi dogo,maana bila ya kujua unachokiamini hautaweza kujua nini mafanikio katika maisha yako,hasa ukiweza kuchagua mambo katika yale yale unayoyaamini,mawazo hasi ndiyo yanayomfanya mwanadamu aweze kubadilika,kwa kuweza kufikiria ujumbe unaokuja pale unapofanya jambo,unaweza kushangaa na bila kujua kwa nini watu huacha kufanya yale waliyoyalenga kuyafanya,je hawajui wanachokitaka?maswali huwa mengi lakini zaidi ni lazima ujue ni kwa nini unakuwa unafikiri namna unavyofikiri,ikiwa kila wazo hasi lina ujumbe wako jiamini kukabiliana na yasiyowezekana

Yasiyowezekana ni yale yaliyopo katika hali ya uwezekano,pengine ikawa chanya,hasi..ikiwa nguvu za kile unachokiwaza ni nyingi ya kuonekana kuizidi chanya,ukicheza salama na kuusoma mchezo vyema unaweza kujua namna ya kujiongeza,endapo ukakubali kwa lolote linalokuja katika maisha yako,endapo ukiangalia kila jambo unalolifanya linaenda katika namna yake na si vile ilivyo katika nafsi yako,pengine ukiwa hujui nafsi ni nini pale inapoongelewa inakupasa kujiongeza,kujua kwingine siyo lazima kufundishwa maana kwa mara nyingine mtu aje akuulize hivi umejuaje..?

Mtu yapasa ujue nguvu ya kuuliza ili kujiongeza zaidi,ikiwa unapouliza ni lazima ujue swali lako litakusaidia nini?pengine unaweza kuuliza swali ambalo jibu unalijua,yote haya huepukana katika kujiongeza,amini hakuna mtu anayekosea maisha kama Yule asiyefanya maisha yake,huo au ule ugumu ni kwa sababu ni maisha pengine ukijiongeza yatakuwa marahisi tu vile unavyotaka,ama kama unaona urahisi ni ugumu basi ongeza ugumu maana dawa ya moto ni moto kama vile tunavyosema.

HAKUNA MKATO KATIKA MAISHA..



Ni kupambana,ni kutia mkazo ili jema la mtu likaja upande wake,maana lako ni lako,maana wewe ni mtu maalum,ikiwa kuna  wakati unaotofautisha maana na kuleta tafsiri tofauti,ukiwa unaishi fanya lile la kesho maana leo imeshatokea pengine ndiyo maana yapasa kujiandaa kabla ya safari,ikiwa kungalikuwa na uwezo wa kutokusafiri kwa kutumia muda basi wengi wasingechelewa,haina maana ya kupita mkato ama njia ndefu ili kuleta neno maisha,ya leo ukiyaacha utafahamu vyema kuhusu kesho,kivingine ikawa ni ufunuo,hakuna mkato katika maisha kwani kila mtu yapasa aishi yake.

Ikiwa kuna kufananisha  ndiyo kumeleta vitu na utofauti,ukitaka kuachia njia yako jaribu kukalili ulipoishia,maana unaweza ukawa hauelewi na kujikuta umeelewa vyema sana kwa kuwa ndiyo njia uliyotaka kupita,unaweza kurudia jambo mara nyingi na usijue ni kwasababu gani haujaweza fanya lingine,hayo yakiwa ni matendo katika maisha yako,jaribu kufikiri nini unataka,chukua hatua na jaribu kupata na kuyaelewa ya nyuma,sisi wote tuna namna moja ya kuishi,ikiwa unaweza kulichukulia jambo kiuhakika katika mlengo wako wowote,upe muda na njia zilizo sahihi,hata ikiwa haujafahamu nini usahihi wake lakini muda utakuonyesha njia,maana utafanya lile linalokusudiwa na muda.

Kama ukienda na kufikiria kila maisha ya mtu mmoja unaweza usione mafanikio maana ni lazima ujue nini unachohitaji katika muda sahihi,pengine yaweza kuwa tumbo linauma kwa sababu ya njaa,fikiri kama unaijua njaa kihalisia,maana hata ikawa gari bila mafuta ni sawa na kumpa baiskeli mtoto asiyeweza kutembea,yote yanawezekana,ikiwa unaweza kukubali kwa yale yanayokupitia maishani mwako.hakuna mkato katika kupika nyama bila maji maana utakuwa unachoma,jambo ni kujua.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...