Thursday, November 15, 2012

JIONGEZE



Endapo hata ukiwa na chaguzi dogo,maana bila ya kujua unachokiamini hautaweza kujua nini mafanikio katika maisha yako,hasa ukiweza kuchagua mambo katika yale yale unayoyaamini,mawazo hasi ndiyo yanayomfanya mwanadamu aweze kubadilika,kwa kuweza kufikiria ujumbe unaokuja pale unapofanya jambo,unaweza kushangaa na bila kujua kwa nini watu huacha kufanya yale waliyoyalenga kuyafanya,je hawajui wanachokitaka?maswali huwa mengi lakini zaidi ni lazima ujue ni kwa nini unakuwa unafikiri namna unavyofikiri,ikiwa kila wazo hasi lina ujumbe wako jiamini kukabiliana na yasiyowezekana

Yasiyowezekana ni yale yaliyopo katika hali ya uwezekano,pengine ikawa chanya,hasi..ikiwa nguvu za kile unachokiwaza ni nyingi ya kuonekana kuizidi chanya,ukicheza salama na kuusoma mchezo vyema unaweza kujua namna ya kujiongeza,endapo ukakubali kwa lolote linalokuja katika maisha yako,endapo ukiangalia kila jambo unalolifanya linaenda katika namna yake na si vile ilivyo katika nafsi yako,pengine ukiwa hujui nafsi ni nini pale inapoongelewa inakupasa kujiongeza,kujua kwingine siyo lazima kufundishwa maana kwa mara nyingine mtu aje akuulize hivi umejuaje..?

Mtu yapasa ujue nguvu ya kuuliza ili kujiongeza zaidi,ikiwa unapouliza ni lazima ujue swali lako litakusaidia nini?pengine unaweza kuuliza swali ambalo jibu unalijua,yote haya huepukana katika kujiongeza,amini hakuna mtu anayekosea maisha kama Yule asiyefanya maisha yake,huo au ule ugumu ni kwa sababu ni maisha pengine ukijiongeza yatakuwa marahisi tu vile unavyotaka,ama kama unaona urahisi ni ugumu basi ongeza ugumu maana dawa ya moto ni moto kama vile tunavyosema.

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...