Friday, November 16, 2012

MAISHA NI VITA.

 Uko vitani jina liko vitani,ili kudondoka karibu au halisi katika nyota liweke jina lako katika mwendelezo wa kuwa JUU pengine unaweza usifikiri kuyatilia maanani yale unayoyawaza kwa kudhani Mawazo yako si bora sana,ikumbukwe utofauti wetu kimwili,maungo maumbile na kadhalika upo hadi katika utajiri maana ni wewe unachagua ukiamua,pengine ukapendezwa na yana au yaliyotokea kutokana na kwamba hayajakupata wewe zaidi,huwezi kuyajua ya adui bila ya kupigana naye vita,pengine hasira haina ufahamu zaidi ya adui wenyewe wa pande zote mbili kujua tofauti zao maana umeumbwa katika namna hiyo ya utofauti

Haki ya kesho ni siku nyingine maana unaweza ifahamu kwanza,pengine mmoja akikupokonya chako hapo ndiyo unaweza jua kweli,pengine ikaja vita nakupigana,hapo bila ufahamu,unapopigana lazima ujue unapigania nini,ikiwa ni ya wengi lazima uangalie kama na yako umeyapigania,katika maisha uwongo ni sumu na kichecheo kikubwa sana cha vita kuliko kitu chochote kile,hapo ufahamu uongo ni nini,hapo mahala kwengine kwa moyo kukiwa wazi na kwengine kukiwa kunasaza,maana vita ni kama mzani.

Huwezi kuelewa mwenzako anapigana nini bila ya wewe kuamua kupigana,ingawa si lazima wote muwe katika vita,wengine hukasirika kwa kuambiwa huwezi kwa kuona unaweza na kuleta vita,wakiwa wachache wenye ufahamu ni wengi wanapoutumia ufahamu wao,maana baada ya kujua wengi ni wachache imekuja kuleta vita na kuondoa amani,ile nguvu ya kwenye ufahamu imekuwa nyingi kwa wengi.

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...