Tusitake ubishi kwa yaliyo matapishi,tusipende upishi kwa
walio wabishi,tumeamka leo mapema ikaonekana ni wabishi,tumefanya leo jambo
jema isije kuwa watishi,watoto chungeni wazazi wenu wanawaona,wakubwa
jiangalieni madogo mumeyaona,tumetoka juzi kufanya bila kujua,tulifahamu juzi
kwa watoto walitambua,mizigo midogo
vyombo vikubwa visije ungua,uadilifu mdogo tuyaangalie makubwa yatatuumbua..
Samaki mkunje akitaka akikatika amezeeka,samaki mbonye akiweza kaoza,ona tumekuja leo bila
kuzoza,wachache jitayarisheni mje kutuongoza,tumesubiri sana tusije
kupuuza,watoto kaeni wazazi kuwatunza,wazazi kaeni chinjo wakubwa wamekuwa,tusiseme
kwa sasa ya kuwa tumejipiga msasa,tusiseme ya sasa kwani yametungoja sana
Vichwa vitakuja na kuwa wangu mkia,watoto watakuwa bila ya
salamu kuwatamkia,haki iacheni mwenyezi akatubarikia,mabaki yaacheni maana
wasije kututapikia,wachache waacheni maana matusi watatutamkia,haki ya nani wa
kwanza kashika mkia,haki ya Fulani wa mwisho atapaswa kutuamkia,adhabu hapewi
mtu akafa akafia,adhabu hapewi mtu yakaja yakamfikia.
Tunaondoka tukienda tukisema,tunaenda tukiondoka
tukihema,mazoezi yamekuwa mazito kwa watoto na kunena,mapenzi yamekuwa mazito
kwa Fulani kunisema,haki hawa watoto wa vizito sio tukiwasubiri tutawasoma,haki
wa kwa watu wenye vibito kwa foleni hawatagoma.mtoto subiri haya magali
yamegoma,ingekuwa kiroboto asingesubiri kwa magodoro kuyachoma.
Ndoto zikamilike kwa watoto,uoto uelimike hata kwa viboko..