Monday, October 9, 2023
Makaya's Forum: NAONA
NAONA
Naona umekalia mguu wako ukijaribu kutupa mkono kulia ili usaidie kusimama na mguu wa kushoto,naona ukiambiwa acha kwa kuwa hujajua kuwa ni moto na unaunguza,Naona vingi ukipata uelewa ntakuelewesha.
Naona wamefunga milango wakijua upo nje,wamefunga njia ikiwa bado haujapita,wanakusema unakonda kwa kukataa kunywa uji,naona ukisoma herufi bila ya kuelewa,umeanza kuita mma ukijua ni uhai,naona chuki juu ya moyo mkunjufu,Subiri ukipata uelewa ntakuelewesha.
Naona hujajua kama sufuria sio kikombe,hujajua mtu anayesubiria hakupata hajapata sifuri,usikimbilie kuendesha vitakavyo kuendesha,subiria kupandishwa basi likisimama utashushwa,Unapokula usijichafue sana meza wapo wabaya watu wanaotafuna vya kumeza.
Naona unaanza kuelewa ya msingi,ukitaka kujisaidia waogope watu na isiwe kwa chuki ,kama umekuwa jua safari unaiweza na unapoelekea naona safari ndo inaanza,Naona unashindwa kufanikiwa kwa fitina nyingi,vita zipo nyingi kaa mbali na maadaui,binadamu yoyote anaweza kuwa adui bila hata wewe kutaka,naona unakuwa msuruhishi mbele ya ndugu zako na sio kuwagandamiza.
Kesho naiona tena,naliyaona ya jana yakanipa majibu ya kuwa mtihani ni ule ule.naona yake akae nayo yako baki nayo mwenyewe ili kutokuchanyikikika,Naona unakanyaga maji na hakuna sehemu yenye moto ,Naona nisikuchoshe Sali sana kaa mbali sana na ndugu msumali.
Makaya's Forum: ELEWA 2
Makaya's Forum: ELEWA 2 : Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...
-
Pengine ukawe umemaliza mambo yako,au ukawe upo katika njia ya kuutaka ufalme,kipindi kile cha ngamia kupenya kwenye tundu la sindano ...
-
Makaya's Forum: AMUA YAKO. : Duniani wengi humkimbia mtu kipindi cha kifo,maana wakiona taabu ndiyo utasikia Yule kachanganyikiwa kabisa...
-
Makaya's Forum: YAFANYE MAPITO KUWA ELIMU. : YAFANYE MAPITO YAKO KUWA NGUVU INAYOKUSUKUMA KWENDA MBELE UKITEGEMEA KUISHI NDOTO ZAKO NA S...
-
Yafanye mapito yako kuwa nguvu inayokusukuma kwenda mbele ukitegemea kuishi ndoto zako na sio kile unachokiogopa na kuhofia,wengi hawafanyi...
-
Duniani wengi humkimbia mtu kipindi cha shida,wanaoamini kufika darasani ni kuelewa zaidi ya maisha yalivyo wameelewa tofauti,ikiwa...
-
Hulazimishwi kulia na wakati wewe unataka kufurahi na kucheka,swala la msingi ni kujua unapokatazwa kulia,hapa nikiwa sina maana ya...
-
Makaya's Forum: MAPENZI YANAISUKUMA DUNIA.. : Usipoelewa hautaweza kujua hata kama unashiriki vipi,maana kwa kutokuyapenda na kujifanya ...
-
Unaweza ukawa unakataa mazingira uliyonayo,ukajikataa ukakataliwa ama ukakatalika hiyo yote ikaonekana kwa kuwa maisha yana msukumo tofaut...
-
Makaya's Forum: NIA NA THABITI YAKO MWENYEWE : Pengine tusije tukaenda madukani tukasema ni akili zetu,hii ikiwa kuna kuagizwa ama kwend...