Thursday, September 13, 2012

VIPINDI...

Ukiwa ni mtoto,pengine ndiyo unazaliwa,ama vile ilivyo ,hapa nikiwa na maana katika maumbile na namna ya vile tulivyoumbwa,pengine wengine wakaumbika,kutokana na kile walichokipokea kwa kutazama kujua ama kutokujua,nyingine zikiwa kama ni sheria za kuishi,ikiwa unaweza kuzipenda ama kuzichukia,lakini hiyo itakuwa ni yako,pengine sababu katika kipindi chote kinachozunguka  maisha yako ,hapo ni lazima kujifunza,tena kujifunza hata kwa kulazimisha kipindi.

Hivyo ikiwa kama umejiunga katika shule,pindi tokea pale ulipozaliwa,katika kila siku ya mungu utapata nafasi ya kuweza japo kuelewa zaidi ni nini kinachofundishwa katika vipindi hivyo,tena kukiwa hakuna makosa ni vipindi tu,hapo ikiwa utavipenda,utavichukia pengine hata kutoa machozi kabisa,hapo ikiwa kuna kukua kwani ni jaribu la kosa na kile kifanyikacho kwa matendo.yale yanayofanyika kwa kushindwa pengine hutokea na kuwa kamili.

Vipindi huwa vinarudiwa mpaka vile ilivyo ieleweke,ikiwa kipindi hicho kimekuja katika namna ya kutaka watu welewe,na baada ya kumaliza ukaelekea katika kipindi kinachofuata.vipindi havina mwisho,hakuna maisha ya mwanadamu yasiyo kuwa na vipindi,kama uko hai basi jua kuna kipindi japo kimesomeka,hata wakati wengine wakiwa kama mahala ambapo kipindi hicho kitafanyika.

ANZA UPYA..

Ni katika kuanza mwanzo,pale ikiwa kuna makosa ama ni njia mpya,ikiwa unahitaji la kuwa peke yako ama kukaa gizani ikiwa jua litawaka kesho,hivyo ni lazima kufanya katika uwezo wako ili inayofuata ije vizuri,pale inapofika kipindi cha kuanza upya,moyo ukiwa na yake kama mistari ya rangi ikiashiria mvua kunyesha pasipo taarifa,ama ni kuzuia endapo italeta uharifu.miaka haita weza kuchukua vile ulivyofanya,ikiwa nafasi ya kuanza upya ni pekee kwa sasa,hivyo bado ndoto zitakuja kweli.

Ukiwa muda uwapo na upweke sio peke yako,njia yaweza kuonekana nyembamba ikiwa hata sauti hazisikiki,pengine sauti ndiyo zikatembeze nafsi,pale unapokuwa peke yako,hiyo ikiwa umeishia hapo unasubiri kile maisha itakuletea,katika kila maisha ikitakikana asubuhi njema,kwa mabaya ya maisha kuyaacha na kuchukua nafasi yako iliyo mpya,pengine ikiwa ni muda wa kufanya vile uvifanyavyo,yaani ipasavyo.

Magumu huwa yanaonekana baada ya kufanyika ikiwa haikueleweka mwishoni utasikia ‘nilijua’maana hata ya kushindwa yanajulikana,na hii ikiwa kwa kufahamu ama kwa vile ilivyo inavyoweza kwa makosa kuyafahamu,maana kwa kipindi kilichopo yahitaji kuwa kiongozi bora ndani ya maisha yako,ukiwa kijana anza kwa kuweza hata kuendeleza maana yote yanayokuja ni baadhi ya yale uliyoyafanya mwanzo.

NJIA INAPOTEA

Kizazi kinachokuja ni kizazi kinachosoma kupitia yale tuliyoyafanya!pengine isitoke lawama kama kuna upotevu wa namna yeyote ikiwa wale wa mwanzo hawakuelewa walichokipata,baada ya kutafuta ama ikiwa vilikuja kibahati,kujitoa kwa moyo mmoja inasemekana kwa sababu kuielewa njia unaweza kuipotea na kujikuta upo sahihi ili mradi ukiwa na tamani ya kutaka kuelewa na kujua,mambo na njia nyingine yapaswa uelekezwe,nyingine ukaelekezwa kwa kupata kwanza na kuikosea baadaye tena  kwa moyo mmoja

Ikiwa haijulikani haina haja ya kujaribu maana itashindikana kurudiwa tena,hiyo ikiwa ni kama fundisho  kwa namna ya kutokujulikana ya kwanza kama imetokea maana kutokujua ni kosa lako,tusijari vipaji maana wote tunavyo,ikiwa msingi ni kuthubutu kwani maisha hayahitaji woga,yakihitaji nafsi yenye kutaka na kutaka kutokupoteza,maana kitu cha mwisho katika maisha yako ni furaha,ambayo umeitengeneza mwenyewe.

Ikiwa kuna mengi ya kuyaweka kichwani na kuyashika,hayatakiwi machache mabovu kuyashika hapo likaja hitaji la kupoteza kwani maana ikaja kwa vile ipo tu,na yaweza kuwepo ikaja kupoteza maana kwa kuwa haikuwa katika uhitaji la wengi,na wengi hao wakiwa wanamahitaji yao,ikiwa hakuna zaidi katika hii dunia ambacho kitafanya tofauti na vile unavyotaka wewe,kama likija tatizo basi ijulikane kuna kukosea na hata kukoseshwa ya kuwa mwanzo haufahamu,

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...