Thursday, September 13, 2012

NJIA INAPOTEA

Kizazi kinachokuja ni kizazi kinachosoma kupitia yale tuliyoyafanya!pengine isitoke lawama kama kuna upotevu wa namna yeyote ikiwa wale wa mwanzo hawakuelewa walichokipata,baada ya kutafuta ama ikiwa vilikuja kibahati,kujitoa kwa moyo mmoja inasemekana kwa sababu kuielewa njia unaweza kuipotea na kujikuta upo sahihi ili mradi ukiwa na tamani ya kutaka kuelewa na kujua,mambo na njia nyingine yapaswa uelekezwe,nyingine ukaelekezwa kwa kupata kwanza na kuikosea baadaye tena  kwa moyo mmoja

Ikiwa haijulikani haina haja ya kujaribu maana itashindikana kurudiwa tena,hiyo ikiwa ni kama fundisho  kwa namna ya kutokujulikana ya kwanza kama imetokea maana kutokujua ni kosa lako,tusijari vipaji maana wote tunavyo,ikiwa msingi ni kuthubutu kwani maisha hayahitaji woga,yakihitaji nafsi yenye kutaka na kutaka kutokupoteza,maana kitu cha mwisho katika maisha yako ni furaha,ambayo umeitengeneza mwenyewe.

Ikiwa kuna mengi ya kuyaweka kichwani na kuyashika,hayatakiwi machache mabovu kuyashika hapo likaja hitaji la kupoteza kwani maana ikaja kwa vile ipo tu,na yaweza kuwepo ikaja kupoteza maana kwa kuwa haikuwa katika uhitaji la wengi,na wengi hao wakiwa wanamahitaji yao,ikiwa hakuna zaidi katika hii dunia ambacho kitafanya tofauti na vile unavyotaka wewe,kama likija tatizo basi ijulikane kuna kukosea na hata kukoseshwa ya kuwa mwanzo haufahamu,

No comments:

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...