Thursday, September 13, 2012

VIPINDI...

Ukiwa ni mtoto,pengine ndiyo unazaliwa,ama vile ilivyo ,hapa nikiwa na maana katika maumbile na namna ya vile tulivyoumbwa,pengine wengine wakaumbika,kutokana na kile walichokipokea kwa kutazama kujua ama kutokujua,nyingine zikiwa kama ni sheria za kuishi,ikiwa unaweza kuzipenda ama kuzichukia,lakini hiyo itakuwa ni yako,pengine sababu katika kipindi chote kinachozunguka  maisha yako ,hapo ni lazima kujifunza,tena kujifunza hata kwa kulazimisha kipindi.

Hivyo ikiwa kama umejiunga katika shule,pindi tokea pale ulipozaliwa,katika kila siku ya mungu utapata nafasi ya kuweza japo kuelewa zaidi ni nini kinachofundishwa katika vipindi hivyo,tena kukiwa hakuna makosa ni vipindi tu,hapo ikiwa utavipenda,utavichukia pengine hata kutoa machozi kabisa,hapo ikiwa kuna kukua kwani ni jaribu la kosa na kile kifanyikacho kwa matendo.yale yanayofanyika kwa kushindwa pengine hutokea na kuwa kamili.

Vipindi huwa vinarudiwa mpaka vile ilivyo ieleweke,ikiwa kipindi hicho kimekuja katika namna ya kutaka watu welewe,na baada ya kumaliza ukaelekea katika kipindi kinachofuata.vipindi havina mwisho,hakuna maisha ya mwanadamu yasiyo kuwa na vipindi,kama uko hai basi jua kuna kipindi japo kimesomeka,hata wakati wengine wakiwa kama mahala ambapo kipindi hicho kitafanyika.

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...