Monday, March 19, 2012

Makaya's Forum: FIMBO YA MBALI HUUA NYOKA WALIO MBALI !!

Makaya's Forum: FIMBO YA MBALI HUUA NYOKA WALIO MBALI !!: Umbali unakadiliwa na fahamu, ikijumuisha macho na namna ya shabaha,shabaha hazitokani na yaliyo mbali ndiyo maana ikawa kwa nyoka kuul...

FIMBO YA MBALI HUUA NYOKA WALIO MBALI.

Ikijumuisha macho na namna ya shabaha,shabaha hazitokani na yaliyo mbali ndiyo maana ikawa kwa nyoka kuuliwa kwa fimbo za karibu,hapa usifikiri kifo kikawe ni kifo cha hatari nacho ni kifo kukiwa  na sababu ya kujikinga hapo itaeleweka ni kuokoka,yaani kutoka katika umbali  na uadui.
ikiwa kwa kusikikiliza na kufuatilia kwa ukaribu unaweza kung’atwa na kutiliwa sumu kali ya hatari.

Kama hauelewi ujue sio wakati wako hapo inakulazimu kuuliza ama kusubiri,na hii dawa ya kusubiri ndiyo kuu zaidi maana inaonyesha uvumilivu,yaani ni namna gani,tena uvumilie ukiwa unajua unachovumilia.ikiwa mwanadamu na yeye anauliwa kwa fimbo huna budi kutumia magongo ama mabomu,nyingine nyembamba zingekuwa ni risasi ndogo ndogo na pengine ilivyo kwa mabomu ukapata taabu maana kuna wale walio mbali,wao hufanya hata wakijua wanakosea kweli yakuwa adhabu wanafahamu na kuona wako mbali haitawauma

kukomaa sio kwamba fimbo haijaingia tena maumivu yanaweza kuwa ni makali zaidi ya aliyetazamiwa akilia,ni namna tu ya kuzifanya fimbo zieleweke,Nyoka hatari kwa mwanadamu humkimbilia ikiwa ni kujikinga,na hapa ndipo inabidi utafute fimbo ya karibu,ujikinge na hata walio mbali hata wakija karibu uweze kuwachapa zaidi ukijaribu kufanya fimbo kuwa mkuki kwa kulenga ya mbali.usifike mbali kwa kuwafikiria hao nyoka,zaidi jaribu kutafuta fimbo imara kwani magogo na yenyewe ni mazito sana na ukifananisha magogo na fimbo hapa  utaua nguvu zako wenyewe maana inaweza fika wakati ukajiandaa kwa shabaha ukifikiri watakuja nyoka hao na wasije,
au wakaja katika namna ile iliyo ya gogo,

Angalia  yaliyopo maana umeyaganga wenyewe,yajayo kwa yaliyo pita haya mengine yanaweza kuwa hayana mwenyewe maana na wenyewe nasikia walishayaganga ni kumwachia  chura vurugu za nyoka ukitegemea kwenda mbali kuitafuta fimbo.baba anapomgombeza mtoto kama hasikii siku ifuatayo inapasa mama akataze,na ikiwezekana agombezwe yeye.nakumbuka usemi usemao mtoto wa nyoka ni nyoka,hii sio kwamba haieleweki nyoka ni nani ila ikiwa na mlengo wa kutaka kufahamika kwamba nyoka hazai chura na ikitokea ivyo basi hayo ni maajabu,vitu vya kawaida havina haja ya kushangaa si kama pale ukatumia fimbo ya Mbali kuuwa Nyoka wa karibu..

by:benson G.Makaya
email:bensonsmakaya@gmail.com

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...