Saturday, February 11, 2012

WALIO BORA..


Ubora ni kama uzuri,uzuri ni sifa ikiwa inaelekea kuzidi ni budi kuwa nzuri sana,au bora sana ikiwa ina maana ya kudumu na thamani iliyopo,kwa hiyo ubora unaweza ukawa katika kitu chochote kile kisicholenga jinsia,aina,wala namna,ubora huwa hauulizwi ikiwa unaonekana pale unapokuwa kwa mtu au kitu husika,ikiwa mmoja anafahamu juu ya ubora wa mwingine anaweza naye huyohuyo akawa haelewi  nini juu ya ubora wake yeye mwenyewe,maana tunaweza kuona tu na tusijifunze kitu,au tukajifunza na tusielewe,maana wengi walio bora nao hujifanya ubora ule ni wao,yaani wameutengeneza wao,ingawa si ya kushangaa kama vile ilivyo kwa mtengeneza wino katika peni,naye yu bora lakini siye aliyetengeneza peni.yu bora katika wino.

Moja iliyo kuu  linalohitajika ni lile linalokuwepo ndani ya moyo wa mtu,ikiwamo nia ya kufanya na malengo yaliyothabiti,uthabiti wa kitu ndiyo ubora wake,ubora haulazimishwi na hasa pale mwanadamu anapohitaji,ubora unaendana na matendo ya mtu,watu au kitu.Vingi vilivyopo huwa vinatakiwa kufanyika tena ikiwa ni kwa ubora ule utokao ndani ya mtu mwenyewe,kwani yale yasiyo bora kwa kutokana na mawazo ya mtu hayo yanatokana na mtu mwenyewe pia,aliyoiwazia.hauwezi kuupata ubora kwa kuiga,kwani unaweza kuiga ule wa chini,

Kuna ubora mwingine wa kuonekana tu,ikiwa sifa nyingi zinatokana na ubora basi ni wazi na sifa zieleweke ya kuwa zinakuja zenyewe,hazilazimishwi,ni sawa na kuulazimisha ubora,ni sawa na kulazimisha mapendo,na tuelewe pale tunapolazimisha sio kwamba ni hali imekuwa ngumu bali tunafanya vile hasa visivyo vya muhimu kwetu,hii yote inatokana na watu halisia,nao wakidhani hata pale tulipo ni tumeenda kuonyesha ubora wetu,labda tuseme wa kushangilia maana wanacheza wengine,ingawa ni kweli lakini ubora wa mtu upo kwa mtu mwenyewe,ikiwa ni wachache tunaweza tusielewe na kwa muda mwingine tukajutia kwa yale tuliyonayo.

Ubora huja mahara popote,hata pale katika ukuaji kwani kila Yule anayekuwa atataka kuonyesha ni kwa namna gani ameweza jambo,tendo linapaswa kusifiwa na aliyetenda pia,kwani kama kuiba ni kosa basi na tujue ni haki kweli kumkamata mwizi na kumpeleka mahakamani,ikiwa anaenda kushtakiwa kwa sifa zake,’maana amekuwa bora sana katika kukwapua mali za watu’.unaweza kusema unyooshe njia ili uishi vyema katika maisha yako,ikaja na wengine wasielewe nini na wapi njia hiyo ilipo,

tutashindwa kabisa endapo tutadhania njia,kwani nazo zimewekwa zikiwa na ubora wake,na ili zionyeshe ubora ni lazima kupoteza ubora,wa mtu mwenyewe,ubora wa mpita njia hiyo kwa maana.Maisha na sehemu zake ndizo zinazofanya usiweze kuonekana bora,maisha yakiwa mazuri au mabaya,au yakawe mazuri lakini katika upande mmoja,yaani ikawe ni mtu mwenyewe anajiona bila kuonwa na ubora,ikiwa sehemu zenye ubora ni chache kuliko watu halisia,

unaweza kurekebisha visivyo bora na kuwa vile namna unavyohitaji ikiwa utajiongoza wenyewe,ukijiamini kwamba unaweza na itafika kipindi utapewa sifa bora,kwani na huwa inafika kipindi hata mwizi huacha licha ya kutamani kuiba kutokana na kwamba anataka ubora na siyo amekuwa bora,walio bora wapo kama mimi,wewe na wengine tofauti ikiwa ubora wetu nao upo tofauti.
Ubora wetu upo pale tutakapouonyesha.’

By:Benson G.Makaya,
Tel:+255 714 33 66 57.
email:bensonsmakaya@gmail.com

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...