Ubora ni kama uzuri,uzuri ni sifa ikiwa inaelekea kuzidi
ni budi kuwa nzuri sana,au bora sana ikiwa ina maana ya kudumu na thamani
iliyopo,kwa hiyo ubora unaweza ukawa katika kitu chochote kile kisicholenga
jinsia,aina,wala namna,ubora huwa hauulizwi ikiwa unaonekana pale unapokuwa kwa
mtu au kitu husika,ikiwa mmoja anafahamu juu ya ubora wa mwingine anaweza naye
huyohuyo akawa haelewi nini juu ya ubora
wake yeye mwenyewe,maana tunaweza kuona tu na tusijifunze kitu,au tukajifunza
na tusielewe,maana wengi walio bora nao hujifanya ubora ule ni wao,yaani
wameutengeneza wao,ingawa si ya kushangaa kama vile ilivyo kwa mtengeneza wino
katika peni,naye yu bora lakini siye aliyetengeneza peni.yu bora katika wino.
Moja iliyo kuu linalohitajika ni lile linalokuwepo ndani ya
moyo wa mtu,ikiwamo nia ya kufanya na malengo yaliyothabiti,uthabiti wa kitu
ndiyo ubora wake,ubora haulazimishwi na hasa pale mwanadamu anapohitaji,ubora unaendana
na matendo ya mtu,watu au kitu.Vingi vilivyopo huwa vinatakiwa kufanyika tena
ikiwa ni kwa ubora ule utokao ndani ya mtu mwenyewe,kwani yale yasiyo bora kwa
kutokana na mawazo ya mtu hayo yanatokana na mtu mwenyewe pia,aliyoiwazia.hauwezi
kuupata ubora kwa kuiga,kwani unaweza kuiga ule wa chini,
Kuna ubora mwingine
wa kuonekana tu,ikiwa sifa nyingi zinatokana na ubora basi ni wazi na sifa
zieleweke ya kuwa zinakuja zenyewe,hazilazimishwi,ni sawa na kuulazimisha
ubora,ni sawa na kulazimisha mapendo,na tuelewe pale tunapolazimisha sio kwamba
ni hali imekuwa ngumu bali tunafanya vile hasa visivyo vya muhimu kwetu,hii
yote inatokana na watu halisia,nao wakidhani hata pale tulipo ni tumeenda
kuonyesha ubora wetu,labda tuseme wa kushangilia maana wanacheza wengine,ingawa
ni kweli lakini ubora wa mtu upo kwa mtu mwenyewe,ikiwa ni wachache tunaweza
tusielewe na kwa muda mwingine tukajutia kwa yale tuliyonayo.
Ubora huja mahara popote,hata pale katika ukuaji kwani
kila Yule anayekuwa atataka kuonyesha ni kwa namna gani ameweza jambo,tendo
linapaswa kusifiwa na aliyetenda pia,kwani kama kuiba ni kosa basi na tujue ni
haki kweli kumkamata mwizi na kumpeleka mahakamani,ikiwa anaenda kushtakiwa kwa
sifa zake,’maana amekuwa bora sana katika kukwapua mali za watu’.unaweza
kusema unyooshe njia ili uishi vyema katika maisha yako,ikaja na wengine
wasielewe nini na wapi njia hiyo ilipo,
tutashindwa kabisa endapo tutadhania
njia,kwani nazo zimewekwa zikiwa na ubora wake,na ili zionyeshe ubora ni lazima
kupoteza ubora,wa mtu mwenyewe,ubora wa mpita njia hiyo kwa maana.Maisha na
sehemu zake ndizo zinazofanya usiweze kuonekana bora,maisha yakiwa mazuri au
mabaya,au yakawe mazuri lakini katika upande mmoja,yaani ikawe ni mtu mwenyewe
anajiona bila kuonwa na ubora,ikiwa sehemu zenye ubora ni chache kuliko watu
halisia,
unaweza kurekebisha visivyo bora na kuwa vile namna unavyohitaji
ikiwa utajiongoza wenyewe,ukijiamini kwamba unaweza na itafika kipindi utapewa sifa bora,kwani na huwa inafika kipindi hata mwizi huacha licha ya
kutamani kuiba kutokana na kwamba anataka ubora na siyo amekuwa bora,walio bora
wapo kama mimi,wewe na wengine tofauti ikiwa ubora wetu nao upo tofauti.
‘Ubora wetu upo pale
tutakapouonyesha.’
By:Benson
G.Makaya,
Tel:+255 714 33 66 57.
email:bensonsmakaya@gmail.com
No comments:
Post a Comment