Leo ikiwa inatakiwa kujijua zaidi ya maana ya
kujirudia,ingelikuwa ni mpya ningesema usihofu lakini haina maana ya kuingoja
wakati ni bure muda unaenda,leo ndiyo siku ya kukwambia maana jana ilikuwa
inaanza kujirudia,tena ikafahamike kwamba imerudi kwa ajili ya kuelewa,tena
kufanya sahihi kwani ni tabia,tabia kila mtu anayo ya kwake,mwanzo ikaonekana
ni makosa yaliyo na samahani kumbe hata wengine walikuwa wakitamani,si wanaujua
ukweli,tena hakuna kubisha maana imejirudia.
Unaweza kujaribu kuwa tofauti na ilivyo lakini mwishowe ni
kukubali maelezo,tena ukahisi kuna usaidizi kwa kujulikana ni bahati mbaya
lakini tabia yako imejulikana,maana ukionekana sijui ni vipi utasema haina
maana,ya kuwa umegundua ni makosa,ni makosa makubwa sana kwa kutokufanya lile usilokusudia,maana
wakati mwingine unaweza kutenda jambo ukihisi umeweza bila ya kujiuliza
yaweza kuwa unayarudia,tena yale yale..
Tabia yako chafu sana maana Ikiwa unajua kama unayoyatenda ni
makosa alafu unatenda,sasa labda uitwe ni mpumbavu,maana kwa vile ya kutokujua
ni mkosa baada ya kufanya kosa,ikiwa mwanzo lilipuuzika tu,hiyo ni tabia ya
binadamu kuchagua njia zao katika kuelekea kifo pia,unachagua wenyewe,unajijenga
wenyewe,maana kuna vitu unaweza kuishi navyo maishani mwako na
usivifurahie,baadaye ukitegemea uvafurahie,inakuwaje usipofurahia milele?maana
kwa hapo tu yanakuwa yamewezekana mengi sana..tena yale yale.
Inatakiwa kiingilio sasa katika kuwekeana tabia njema,hapo ukianza tangu utoto,hakuna Yule mwenye tabia nzuri kati yetu wote humu
duniani zaidi ni wote tunayajua mema ni yapi na mabaya ni yapi,hapo haikuwa na
maana ya kusema mimi,kizuri ni kile cha mtu chake maana mkubwa anasema ili
mtoto afuate tabia fulani,tena ikiwa mkubwa amekuwa katika tabia fulani..uelewa
ni swala tofauti na tabia,maana tabia ni wewe,ndiyo maana hakuna kama mungu,ni
yeye lakini yu ndani yetu,yupo kama sisi,yamkini yeye ni mkuu.yeye anatabia
zake..