Tuesday, March 27, 2012

NAFSI HURU


Namna tunavyoweza kujitambua  katika kufikiri na vile ilivyo kwa kuona na kusikia.basi nafsi inaweza kuwa roho.Kuweza kujitambua ni kuwa na utambuzi,utambuzi wenye mtazamo halisia na Yule mwenye nafsi.nafsi huru ndiyo ile inayofikiria mema juu yake,ikiwa mema ni yale ya mtu mwenyewe hivyo tunafika na kuona namna nyingi za kuifanya akili  yako kuwa katika mtazamo ulio bora kupitia nafsi.

Usichukulie vitu ki mimi zaidi, hapa nikiwa nina maana ya ubinafsi,wengi wetu hatulewi nini ushirikiano lakini ukitegemea kwa kutofanikiwa kwa yale unayofanya peke yako,sijui ingekuwaje kwa jinsi ungevyomlinda Mungu kama ingelifahamika tu kila mtu amekuja peke yake na wake,yaani haieleweki alipotokea ni mshtuko na kukutwa yupo akinyonya maziwa yaliyoshushwa mbinguni,ingelikuwa ni hatari sana kumzidi kuweza kufikiri mmoja wapo asiyenyonya  lakini si  katika nafsi ya pili na kuona katika jicho la tatu.

   Sahau yako yaliyopita yale ya zamani.ndwele,ikiwa sio mazuri au mabaya kinachohitajika hapa ni kuweza kusahauika ,ni mengi zaidi yanayokuja hasa tukiangalia na yenyewe yanahitaji akili na nafsi zetu hizi hizi ili kuwezakufikirika,binadamu ana aina ya matendo pale inapomkutia nafsi yake,sipendi kumsingizia mungu lakini kwa mwanadamu lolote lina haki kutokea mbele yake ikiwa  ilipangwa kuishi hivyo inatupasa kusahau inapobidi na zaidi ni kuweza kufikiri yanayobidi.
.
   Kubali yale yasiyo badilika kubali kuna yale marahisi,kubali kuna yanayowezekana,ikiwa yamewahi kuwezekana kwako basi kubali pia kuwa kuna yale yasiowezekana maana ingalikuwa hivyo tungefanya vyote wote tena bila kujali,magumu mengi huchanganya wanaadamu hivyo kufanya hata kuchanganyikiwa,hapa haina haja ya kuchanganyikiwa endapo utafahamu kuwa yapo ambayo hayawezekani katika nafsi yako.

   Kuwa mvumilivu…hatuwezi kusema uvumilivu ndiyo kila kitu kwani hata tukiuvumilia moto mwishowe ni kuungua tu,hata ukavumilie mazuri kwani mabaya ni yapi?uvumilivu unahitajika katika watu pamoja na maeneo pia.huku akili timamu ikitangulia kutafuta majibu sahihi pakiwa na uhuru ndani ya yako,uvumilivu ni njia ya ushindi pale unapotakiwa , unapaswa kuwa wavumilivu ili kuweza kujua hasa ni nini zaidi ambacho kinapasa kuvumilika.

 Kaa mbali na wale wanaowaza tofauti na vile utakavyo  wala hapa tusitengane wala haina haja ya kubaguana,la msingi zaidi ni kuweza kuwaza ilivyo tofauti na vile wanavyowaza wachache wale wa tofauti,na lengo liwe ni kutaka kuleta utofauti tu,na badaye kuwa bora katika utofauti huo,
maana unaweza kuona kuwa Fulani yupo tofauti kumbe naye anaona swala hilo ni lipi na upande wake kwako pia.

    Nafsi yenye vita ina wivu..wanasema  wivu hudhihirika katika mapenzi ya ukweli,hapa upendo umeonekana ni bora zaidi maana unawezaje kuwaonea wivu wale watu unaowapenda?wivu hautakiwi kokote kwani ni sumu,tunasema sumu ni sumu tu haina idadi ya kua ni nyingi ama ndogo hapo matokeo ndiyo husema,na  wivu usiwe mwingi,hapo utavuna mengi zaidi.nafsi yako itadhurika

    Usiweke na toa kinyongo nafsini,Weka Nafsi yako huru..moyo unamengi sana ya kufanyia kazi ,kipindi unaweza kukuta mwanadamu anataka kujiua hiyo ikiwa ni namna ya mashambulizi aliyokumbwa nayo  katika sehemu yake maana uwanja wa nafsi ni mmoja lakini namba tofauti.watu tupo tofauti.hivyo katika yale ya kuumia zaidi iwe ki hasara ama faida yatupasa kuondokana nafikra hizo chafu na nzuri katika upande wa mtu husika ili kuwa huru. katika mawazo uliyonayo.

 Punguza muda wako katika kuangalia tv na kusoma magaeti muda ulionao ni kwa kuwezesha mambo  kwenda katika mtazamo ulio bora hivyo yapasa kuimarisha ubongo na sehemu zake nyingine kwa kuweza hasa kusoma na kuangalia matukio na vitu mbali mbali ambavyo kiharisia vina punguza kasi ya akili katika kufikiria mambo yasiyo kuhusu na zaidi kujishugulisha na kwa nini sio mimi,hiyo ikiwa ni kama njia moja ya mafanikio binafsi maana akili njema hufuatana nayale inayoyafikiria.

       Jishugulishe fanya mazoezi.vile ilivyo maazoezi sio lazima kunyanyua vitu ambavyo ni vizito labda lakini unawezakufanya mazoezi marahisi yatakayo weza kukufanya kuwa katika mtazamo Fulani,
yaani ikawe unafanya mazoezi huku ukifikiri hayo mazoezi katika kuujenga na kuimarisha miili yetu.
unapoimarisha mwili wako  unaimarisha nafsi yako

  Jifunze namna ya kuweza kukaa kimya na kufikiri juu ya maisha yako.muda mwingi huwa tunakaa hasa tukitafuta maisha lakini nafsi na akili zetu zikiwa baado hazina utulivu,hapa tunashauriwa kutulia kwa muda na sio bila kuongea lakini pale inapobidi hii itasaidia katika kujua yale mazuri kwa upande wako na yale mabaya pia.


By Benson G.Makaya

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...