Sunday, August 12, 2012

TAARIFA...


Inapofika wakati huwa ni kujiandaa na kusikiliza yale yaliyojiri,
maana kama ni taarifa zimekuja katika wakati wake muafaka,tena wale wanaosoma taarifa yenyewe imewapasa kuwa kufanya vile wanavyoweza ali mradi hali ikaeleweka,maana kuna kutengeneza.mengine yakifika hufanya watu kuwa na mshtuko kutokana na taarifa zenyewe pengine kuwa ni mbovu sana ama zimependezesha hali iliyopo,unapopokea taarifa si lazima kusema ama kufanya vile utakavyo zaidi ya kufuata maelekezo,maana hata tukadanganywa kwa taarifa zisizo na ukweli taarifa zinakuwa zimekamilisha lengo lake.

Hapo tunaona wanadamu na mambo yao adimu,maana katika swala la kuvaa suti na kandambili huko ni kutokujiandaa,ikiwa unataka kupeleka taarifa za maisha yako ili watu waweze kujua mwenendo wako.pengine ipatikane taarifa nzuri zaidi kuhusu yaliyopo,maana ingawa hali inajaribika kurekebishika lakini inaleta ugumu kutokana na taarifa kutokuwa sahihi,pale wale wachache wakaamua kusema na kujisahau kwa vyeo walivyonavyo kwamba ni wasemaji

Leo tusitegemee mazuri ya kuwa tumeamua kuishi,
pengine tusitegemee kwa kuwa haitaweza kutokea,au ilitokea lakini haikufahamika kutokana na taarifa kuwa mbovu,wale wenye haraka wamefoji ili mradi wao wakaweza kuishi watakavyo,tena bila ya kuamini hata taarifa walizokuwa nazo kabla ya kutoa taarifa zao zilikuwa za uwongo,kwa kutimilisha hayo ikawa hakuna njia ya kutokea,ni sawa na pale unaingia katika mpambano wa ngumi na hata hujapigana mpito mmoja unatoa tamko la kushindwa kutokana na taarifa zilizosikika kwamba mpiganaji  mwenza huwa anapiga ya kuua kabisa.ni katika baadhi ya taarifa,pengine wewe ndiyo unasubiriwa ili utuletee taarifa njema.

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...