Ni namna ya maisha yanavyokwenda,maana leo ikaja lakini siyo
kesho,ukawa na hofu ya leo maana ile ya jana nusu imeishia leo.. kama ilikuwa
ni chuki wazi ukawa na wasi wa kesho kuja na kukudhuru tena,usiogope kwa kuwa
haujui,na tena kuwa na furaha kwani ukijua hautaweza kuogopa,hivi muda
unavyokwenda unapelekwa na wewe,hivi kesho giza baadaye ujue unaileta
wewee...mwangaza wa kung’aa humulika mbali kwa kuwa huitaji kukumulikia,ikiwa
mazuri unayaogopa basi kuwa na furaha na mabaya ya baadaye.
Muda wa kutokuzungumza utafika,ile shule ya maisha yako
ukaja kuijua shuleni.tena ukajifunza mawili kwa kuogopa kujua lako moja,leo ukiwa
unajitahidi kesho utaweza maana njia ya mpita njia hueleweka yake kwa kuwa
hupita kila siku hapo kwenye njia yake,pengine ikiwa ni mara chache acha jina basi,maisha
mengine hayajulikani,hayo ndiyo maisha yako,pengine ukitaka kuyabadilisha ni
uyabadilishe hapo ulipo,ujibadilishe,ukaogopa kupangua kwa sababu ya uwingi wa kushindwa
kupanga tena jua unaidhurumu furaha yako,dhuruma mbaya maana hitaji lake wakati
wa kurudi ni FURAHA.
Sitaweza kuogopa kukwambia ukweli kwani naihitaji furaha
yangu baadaye,kwa Yule anayeogopa kwa kusema uwongo wakati ukweli upo,hafai
hata kujifunza jambo,maaana ataangamiza jamii kwa kutengeneza siraha inayodhuru
bila woga.pengine usiogope kusema utakavyo maana hautaishi tena,kama ikiwa ni katika namna tofauti,hata kama umewahi kusikia pale mtu akisifia “ahh yale
siyo maisha”..yapo yale yaliyo ni maisha pengine kama ulikuwa unaogopa kuuliza
ijue furaha yako.
No comments:
Post a Comment