Saturday, November 10, 2012

SHUKURU KWA YOTE..


Hapa  akihusishwa Mungu kwanza maana kila mtu anayajua yake inapaswa kushukuru kwa kuwa ni kazi nzito umeifanya,Asante Mwenyezi Mungu.
Ukiwa una uelewa ni lazima kubaki katika njia ambayo wewe mwenyewe unaiona siyo ya mapumziko maana ni lazima kutoa nguvu  Pamoja na akili yako ukiwa umeamka na kuchagua kile ambacho wewe umetaka kukiangalia,ukichagua lile ambalo limekuja katika muda unaofaa kimaendeleo,ikiwa maisha ni sehemu inayofanya ndoto kukamilika,ki imani ikiwa kama ndoto ni jibu la tatizo.pale unapomaliza jambo yapasa kushukuru kwa kuwa linakuwa vile kidogo ya ulivyofikiri,huwa yanafanana lakini rangi tofauti na kuthaminisha kule/kile/vile ulivyofanya.


Kama una ndoto ya kuwa  na furaha ama vile katika hali isiyofahamika,kama unapofumba macho ukitegemea kuona chochote mengine yatapita yakiwa ni afadhali kwa kuwa yatastahiri kukuchanganya,shukuru kwa kuwa siyo yote unayoyategemea hutokea ,mengine yakiwa yameletwa maksudi ili mradi na wengine wakapata shukrani za lazima,lakini ikiwa kama mtu ameamua kufa kwa kujinyonga akipona hastahiri kushukuru kwani lengo lake halijatimia.


Pongezi kwa shukrani iliyomaliza jambo,hongera hutoka pale shukrani inapokuwa na jibu lake katika jambo husika,maana katika namna ya kuzaliwa kwa sisi waswahili zinaweza kuwa ni kejeli,ikiwa unataka kuona ni nini unachokifanya haistahili kuuliza bila ya kuulizwa,hapa itatakikana kuonekana mwisho ikiwa unakipaji chochote cha kufanya hakitaweza kulinganishwa na muangaliaji ama yule asemaye kwani mwishoni huja na kukuvisha taji.mawazo yako ndiyo mtaji shukuru Mungu wako alikuumba wewe. hata ungali muda bado kuisha.

No comments:

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...