Tuesday, April 3, 2012

Baniani mpigeni upati wake mpeni..

Katika kuangalia kabila labda tuseme aina naona wao ndiyo wangekuwa na kutokana na nyani maana hata majina na maneno yazungumzwayo yanaashiria hivyo, ni kama pale watoto walalapo wawili katika kitanda kimoja na mmoja akakojoa pale kwa Yule mmoja kumsingizia mwingine ni kazi ndogo sana,yametokea mengi sana na mengi yao mnayajua,ikiwa mengine siyajui natumai hata kiatu changu mtanipa maana haki kumdhurumu mwana vyote si  sawa,

Hapa umekuja kujifunza mengi mengine ambayo yanahitaji chaguzi ambazo na zenyewe zikajichague,Yule asiyeweza mara nyingi hutaka kumkataza mwenzake kwa kuwa yeye amehisi ameweza zaidi,hii ikiwa ni namna ya ulivyoumbwa pale ukawe na kuaminiana pengine ikawe ni kwa sababu ya kiatu tu,ati ya kuwa nawe au Yule naye alikuwa ni baniani,kwangu hilo halina pingamizi maana nakubari kuyaona machache ya watu na yaliyo mengi katika upande wangu.Katika yale yaliyokuwa mazuri wengi wao wameyatafuna,wengine wakavae vizuri na wao wakatake kugawana ikiwa wamekuwa weusi kama ilivyo kwabaniani huyo mwenye chake,wakatake kuchukua hata kile ulichowachangia watu na ikafike mahala pako na penyewe wasemehapa kwetu maana wengine husema mawazo yao kwa kile wanachokifikiria ,hii ikiwa wao wachache kujiona zaidi na bora kuliko ubora wenyewe.

Hapa duniani tumekuja wachache sana na laiti kama ningalifahamu nimekuja na mtu basi hakikanisingemuacha maana kwa walio baki wote wameonekana wanaweza,si wana viatu..
hii ikiwa ni kwa macho na uwezo walionao,hapa naogopa kusema ingawa nitakuwa kama wao,eti mara nyingine ni sisi tunaosema maneno ya watu na hata usifanye.nimempa chake Yule mwenye nacho maana kile kilicho na uchafu wake ni hitaji la jalala Hakuna majigambo mbele ya ukweli,hapa utazamane na usemezane,ile iliyo na ukweli si vibaya kuambiana maana kwa pengine ukataka sifa zisozo kuwa na maana zaidi ya upumbavu,na hili ikiwa walewale wapumbavu ndio wanashabikia,siku hizi hakuna cha wakubwa maana wao ndiyo wamefanya hivi,walikataza kuokota cha jalalani lakini alikutwa mkubwa mmoja akila,aliwaza na mwengine kumfuatia,tena bila ya umakini kwa maana kama angelianza hivyo tungefahamu,

Hata kushindwa ni kuweza pale ikaja kwa mmoja Yule asiye fanya na hata Yule aliyetaka kufanya katika namna yake,hiyo ikiwa inatakikana kuangaliwa katika mtazamo wake..
hapa wengi watasema ikiwa na wale wanaovaa miwani kama mnawakumbuka,maana hao huona marambili zaidi ya vile kuona,kama angali bado haja ona basi na yenyewe huwa ni mara mbili zaidi angali hajaona,hapa usibishane ikiwa muda haujatambulika,ingalikuwa miwani yenyewe ni hii tuivaayo hakika hata hakika ungalitafuta hata iliyo na muundo wa mbao,na hata kioo kisiwepo maana huwa wanasema kinakutazamisha tofauti na namna ya vile utazamavyoufikiri kwa wasio ona kabisa labda,maana wao ndiyo wangepewa lensi kali zaidiIkiwa haki yako umeishindwa kuipata hata kwa kuvua kiatu na kukaribishwa ama ilivyo kwa maji kunawa kijapo chakula basi jiandae…jiandae kupata vitu hivyo maana ilikuwa ni zamu ya kuwachangia wengine na sasa ni yake,upatu huu…umwangalie mbaya maana baniani yu karibu yake.

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...